Pages

Tuesday, April 14, 2015

Diamond amesema ujauzito Zari aliobeba ni kama kamuweka kiganjani..Hakutegemea kuwa na Zari

MSANII wa Bongo Fleva, Nassib Abdul (Diamond Platnumz), amesema ujauzito aliobeba Zarina Hassan ‘Zari’ anaona kama amewekwa kwenye kiganja cha mchumba wake huyo.

Diamond alisema licha ya kutokuwa na fikra ya kuwa na maisha ya kujenga familia na msichana huyo wa Uganda, ila ujauzito alionao unaotarajiwa kumletea mtoto umekuwa chachu kubwa ya kuongeza mapenzi kwa Zari.

“Sikutegemea kuwa na Zari, lakini kwa hali aliyonayo sasa ya ujauzito ni kama ameniweka kiganjani na sasa ninachoomba mtoto azaliwe salama na awe na akili nyingi,’’ alisema Diamond.

Diamond aliongeza kwamba wasichana wengi aliowahi kuwa na uhusiano nao walikosa vitu vya kufanana naye.

“Niliokuwa nao nadhani kulikuwa na vitu ambavyo havikukamilika, ndiyo maana hatukuwa tukiishi kwa muda mrefu na kuanzisha maisha kama haya na Zari,’’ alisema Diamond.

MTANZANIA

No comments:

Post a Comment