Pages

Monday, April 27, 2015

H Baba amesema baada ya mkewe Florah Mvungi kujifungua hivi karibuni mtoto wa kiume anayeitwa Afrika, mkewe huyo ataachia filamu mbili kwa mpigo.....Walipanga wazae watoto wawili kwahivyo mipango imetimia

Mtoto wa kwanza wa wanandoa hawa anaitwa Tanzanite..
Baada ya kujifungua mtoto wa kiume aitwaye Afrika,mwigizaji wa filamu za Kibongo,Florah Mvungi amejipanga kuachia filamu mbili kwa mpigo.

Mume wa msanii huyo,msanii H.Baba
akizungumza kwa niaba ya mkewe alisema kuwa kwa sasa yeye na mkewe ni muda wao wa kufanya kazi kwani wana mpango wa kuachia filamu mbili mpya kwa mpigo ambazo hajazitaja jina.


‘Unajua tulipanga tuzae watoto wawili tunashukuru mipango yetu imetimia sasa ni muda wa kufanya kazi,nitaachia ngoma yangu mpya hivi karibuni na mwenzangu ataachia filamu mbili mpya,’alisema H.Baba.
CLOUDS

No comments:

Post a Comment