Pages

Thursday, May 21, 2015

Christian Bella Amesema Hatumii Madawa ya Kulevya..

Mwanamuziki na mmiliki wa Band ya Malaika Band Christian Bella alimaarufu kama King of melodies amefunguka na kusema kuwa kwa msanii au mtu yoyote yule hawezi kuwa katika nafasi yake ile ile kama atajiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya na kula unga, Christian Bella amefunguka hayo jana alipokuwa akichat live kupitia ukurasa wa facebook wa EATV katika kipengele cha KIKAANGONI ambacho kinafanyika kila siku ya Jumatano kuanzia saa nane mchana mpka saa kumi Alasiri.

Christian Bella aliweka wazi kuwa yeye si mtumiaji wa madawa hayo kama ambavyo baadhi ya mashabiki walivyokuwa wakidhani kuwa huenda anatumia madawa ya kulevya, na kusisitiza kuwa kama angekuwa nui mtumiaji wa madawa hayo basi ni muda mrefu angekuwa ameshapotea kwenye ramani ya muziki sababu muziki kwa sasa ni kazi ngumu ambayo inachangamoto kubwa zaidi, hivyo inahitaji umakini na kujituma zaidi na kudai kuwa hizo ni tetesi zisizo na ukweli wowote.

Msanii Christiana Bella ambaye ni baba wa watoto 2 amewataka vijana wa kitanzania kujituma katika maisha na kutokata taama kwani ipo siku maisha yao yatabadilika na kupata mafanikio kama watakuwa wakijituma, lakini pia amewataka wanafunzi kutoacha shule na kukimbilia kufanya muziki.

"Vijana wasikate tamaa wajitume hata kama maisha magumu wajitume kuna siku tu maisha yao yatabadilika, na kuwa na mafanikio lakini pia vijana wasiache shule sababu ya kufanya muziki sababu Elimu ndiyo kila kitu katika maisha ya leo ingawa wapo vijana wengine wanaacha shule kwasababu ya umaskini hela ya ada hamna ila wanao acha shule wazazi wao wanauwezo wakuwalipia ada niuzembe wa juuu wasifanye ivyo elimu ndo kila kitu."

WASANII WA RNB ANAOWAKUBALI BONGO
Mkali huyo wa masauti alionyesha mapenzi yake kwa wasanii wa kuimba hapa bongo ambao anawakubali na kusema kuwa msanii kama Ben Pol ni moja ya wasanii ambao anawakubali na kuwapenda kutokana na utendaji wao wa kazi na uimbaji wao, lakini pia aliongeza kuwa mwimbaji mwingine Steve Rnb pia anamkubali na kumaliza kwa kusema kuwa hata Jux anajitahidi katika uimbaji wake.

MAHUSIANO KATI YAKE NA NYIMBO AIMBAZO
Mashabiki wengi walitaka kujua kama msanii huyu anaimba vitu amabavyo vinamtokea katika maisha yake au anaimba tu ili kutoa burudani kwa mashabiki na majibu yake yalikuwa kuwa wimbo wa Msaliti ni jambo la kweli ila halikuwa kwake bali jambo hilo lilimkuta rafiki yake wa karibu, lakini pia wimbo wa hamna kama Mama ni wimbo aliomba maalumu kwa ajili ya mama wote ila kilichompelekea kuimba wimbo huo ni pale aliposhuhudia mateso aliyokuwa akipata mkewe wakati anajifungua maana alimshuhudia live mwenyewe.

UTOFAUTI WA MUZIKI WA BONGO NA CONGO
Mkali huyo wa masauti ambaye anashukuru sana kwa yeye kuweza kutoka Tanzania na kuweza kufahamika alieleza kuwa muziki alianza akiwa na miaka 10 Kinshansa na sasa ameanza kupata mafanikio ya muziki wake akiwa Tanzania, na kueleza kuwa kuna utofauti katika muziki wa Congo na hapa Tanzania na kudai kuwa muziki wa Congo ni mgumu zaidi ya muziki wa hapa Tanzania
" Game ya muziki wa Tanzania na congo ni tofauti ya congo iko juu zaidi ila najivunia sana kupata umarufu Tanzania"

"Nilianza muziki congo kinshasa nikiwa na miaka 10 hivyo naweza sema nimeanza kuimba nikiwa mdogo ila show kubwa kubwa nimeanza kufanya mwaka 2002 na Tanzania nimekuja 2006. Nilianza kujulikana na ngoma ya Yako wapi mapenzi ilikua mwaka 2006 ila kupiga hela nimeanza kupata pata hela mwaka 2011 , 2012 nilipo acha Akudo na kutoa wimbo wa usilie , Msaliti, Nakuhitaji , Nani kama Mama , Nashindwa nk hapo ndio nikatoboa na watanzania kunielewa." 
Aliongeza Christian Bella
SIPENDI MAJUNGU NA UFITINA

Mkali wa masauti Bella amefunguka na kusema kuwa yeye katika maisha ya kawaida anapenda amani na kitu ambacho hakipendi katika maisha yake ni ufitina na majungu, hivyo amesisitiza kuwa wasanii wa bongo ambao wanaendekeza majungu na kupigana majungu katika kazi zao waache tabia hiyo sababu kufanya hivyo kunaweza kusababisha amani kukosekana kwa mashabiki au hata kati ya msanii na msani.hivyo amewataka wasanii hao kufanya kazi ya kuelimisha jamii na kuacha na majungu sababu ni dili tena.

Lakini mbali na hilo Bella alisema kuwa yeye mafanikio yake na kila kitu chake kwenda vyema ni kutokana na kumtegemea Mungu kwa kila jambo ambalo anakuwa anafanya .

Mungu ndiyo kila kitu changu namuombaga kila siku anilinde anipe baraka na uwezo wa kufanya vizuri atusamehe zambi zetu amin.
EATV

No comments:

Post a Comment