Pages

Thursday, May 7, 2015

Irene Uwoya kuyaanika maisha yake......Na hivi ndivyo alivyoanza..

MWIGIZAJI Irene Uwoya amesema anajiandaa kuweka wazi historia yake ya maisha maana kuna watu wanapotosha mashabiki wake kwa taarifa za uongo ambazo hazina uhusiano na maisha yake halisi.

Uwoya amesema atafanya hivyo kwa kuwa anataka mashabiki wake waelewe maisha yake halisi na wawapuuze wanaompakazia kwa historia za ajabu zenye lengo la kumchafua na kumrudisha nyuma katika kazi zake na uhusiano wake wa kimapenzi.

“Nitayaanika maisha yangu halisi ili wote wanielewe vema na waachane na kunichukulia tofauti, maana naamini najijua mwenyewe nilikotokea na namna ninavyoishi, hivyo nitaweka wazi ili watu watambue maisha yangu na sipendi watu wanizungumzie kwa kuwa hawayajui maisha yangu,’’ alieleza Uwoya.

Kutoka kwenye ukursa wake mtandaoni,staa mrembo Irene Uwoya ameanza hivi;

Naitwa Irene pankras uwoya...ni mtoto wakwanza katika familia ya mzeee uwoya yenye watoto 2 na mdogo wangu wakuite aitwae babu!!!nimezaliwa dodoma hospital nimeishi dodoma nikasoma shule ya msimgi mlimwa la kwanza mpaka la tatu...Wazaz wangu wakaa mishiwa Dar kikazI mama yangu akiwa ofisi ya waziri mkuu huku baba yangu akiwa pilot na pia ofisi ya nishat na madini nikaamia shule ya msingi bunge na kumaliza la saba!nikaenda kidato cha kwanza St.Thomas Gongolamboto mpaka kidato cha pili badae nikaenda Uganda nikasoma mpaka kidato cha 3 nikarudi bongo kuchukua pass mpya coz ya kwanza ilikuwa imesha isha.....Ilikuwa ijumaaa nikiwa nimeenda kwajili ya pass mpya nirudi shule!!!ndipo nilikutana na kaka mmoja mrefu,mweusi akaniita malaika"nikashangaa mhh mbona sio jina langu ?akanisogelea a kanambia kwa lugha ya kingereza naitwa Patrick ponce monzanga!nikawa na nashangaaa coz sikuwa namjua'nikamwambia naitwa Irene akanambia naomba nikwite malaika coz ur sooo beautiful huku akinipa mkono...nilipo mpa mkono tuuu basiii kumbe nilikuwa nimejitengenezea bomu bila kujua.....ITAENDELEAAAaaaaaaaaa

No comments:

Post a Comment