Pages

Wednesday, May 13, 2015

Jaribio la Kumpindua Raisi Pierre Nkurunziza Burundi


Umati wa watu wakiwa karibu na kituo cha redio na televisheni vya taifa RTNB, Mei 13 mwaka 2015.

Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani.

Hayo yanajiri wakati Pierre Nkurunziza anashiriki
Jumatano wiki hii mkutano wa kikanda wa marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu mgogoro unaoendelea nchini Burundi.

Burundi imekua ikishuhudia maandamano ya raia wakipinga muhula wa tatu wa Pierre Nkurunziza. Kwa muda wa majuma kadhaa mitandao ya kijamii imekua imefungwa, lakini baada ya mapinduzi hayo mitandao hiyo imefunguliwa.

Kituo cha redio RPA ambacho kimekua kimefungwa tangu maandamano hayo yaanze, kimeanza kupeperusha matangazo yake baada ya mapinduzi hayo, hata redio za kibinafsi mbili ambazo ni Bonesha Fm na Isanganiro, ambazo matangazo yake yalikua hayasikiki mikoani na katika baadhi ya maeneo ya nchi jirani, kwa sasa matangazo ya redio hizo yanasikika.

Mapema Jumatano asubuhi, raia kutoka wilaya zote za mji wa Bujumbura walikua wakijaribu kuingia mjini kati Bujumbura, bila mafaanikio. Lakini kuna kundi la wanawake na wasichana ambao wamefaulu kuingia kwenye eneo la Uhuru mjini Kati Bujumbura.

Hata hivyo Ikulu ya rais imetangaza kupitia akaunti yake ya twitter kuwa mapinduzi hayo yamefeli, baada ya jeshi kuingilia kati na kudhibiti hali ya mambo. Hata hivyo raia wameingia kwa wingi mjini kati Bujumbura baada ya kusikia tangazo hilo, huku askari polisi wakionekana kuingia katika makambi yao.

Wakati huo huo wanajeshi wengi wameonekana wakiizingira redio na televisheni vya taifa pamoja na uwanja wa ndege wa Bujumbura.

RFI

No comments:

Post a Comment