Pages

Saturday, May 2, 2015

Mkulima ahukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa kumbaka binti yake......Alimpeleka nyumba ya kulala wageni ndipo akambaka kwa nguvu

Mkulima wa Kijiji cha Waama, wilayani Hanang’ mkoani Manyara, Pachal Yoya amehukumiwa jela miaka 30 baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mapenzi na mtoto wake.

Mkulima huyo anadaiwa kufanya
unyama huo na binti huyo (jina linahifadhi) katika nyumba ya kulala wageni.

Katika hukumu ya kesi hiyo namba 90 ya mwaka 2013, Hakimu wa Mahakama ya Mkoa wa Manyara, Gabriel Ngaeje alisema mtuhumiwa amepatikana na hatia dhidi ya Kifungu cha 158, Kifungu Kidogo cha 1 (b).

Awali, Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Wandiba Wambura alidai Mahakama kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Septemba 23, mwaka 2013 kwenye chumba E cha nyumba ya kulala wageni ya California iliyopo Katesh.

Wandiba alisema kuwa siku ya tukio, Yoya alitoka na watoto wake watatu kwenye kijiji hicho na kwenda Kijiji cha Gitting kumsalimu mjomba wao.

“Baada ya kupanga chumba, aliwanunulia chakula watoto wake na baadaye kuwataka kulala bila nguo,” alidai Wandiba.

Alidai kuwa baada ya watoto wengine kulala, alimtaka binti yake kuvua nguo, jambo ambalo binti huyo hakukubaliana nalo.

“Alipokataa kuvua nguo, baba yake alimvua kwa nguvu na kumtishia kama atakataa kufanya anachotaka atamuua kama alivyofanya kwa mama yake mwaka 2007,” alisema.

Aliendelea kudai kuwa Agosti 29, mwaka 2013 mtoto huyo alimweleza mama yake mkubwa kuwa alibakwa na baba yake, ndipo walipokwenda kutoa taarifa polisi na mshtakiwa kukamatwa na baadaye kufikishwa Mahakama kujibu mashtaka ya ubakaji.

MWANANCHI

No comments:

Post a Comment