Pages

Wednesday, May 13, 2015

Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania aliyejiuzulu hivi karibuni amepata kazi kwenye kampuni nyingine ya mawasiliano nchini Qatar

Aliyekuwa Mkurugenzi mkuu wa Vodacom aliyejiuzulu hivi karibuni Rene Meza amepata shavu katika kampuni nyingine ya mawasiliano nchini Qatar ijulikayo kama Ooredoo Mynmar kuwa Mwenyekiti mtendaji wa tawi la Mynmar.
Aidha, taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na kampuni hiyo imesema kwamba Rene Meza atachukua nafasi ya Ross Cormack ambaye anatarajiwa kuachia nafasi hiyo mwaka huu.

Kwa mujibu wa mtandao wa Afrika Kusini umebanisha kwamba Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom amejiuzulu ili kufanya kazi nyingine.


Hata hivyo mitandao ya kijamii mbalimbali nchini Tanzania imehusisha kuondoka kwake na kashfa ya upotevu wa takribani bilioni 700 fedha za kitanzania ambazo ni sawa dola za Kimarekani milioni 350.


Taarifa hizo zinaarifu kuwa bwana Meza alikuwa kwenye ‘kitimoto’ cha maofisa wa juu wa Kampuni hiyo akihusishwa na kashfa ya kupokea dola milioni 5 kutoka kwa Mmiliki wa Shivacom,Tanil Somaiya ambaye alimpa ili kumziba mdomo kutokana na kashfa ya uzalishaji, usambazaji na uuzaji wa vocha bandia zilizokuwa zinajulikana kwa jina la "Jero jero".


Rene Meza alijiunga na Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom mwaka 2011 akitokea kampuni ya Bhati Airtel Ltd ya nchini Kenya.


Ifuatayo ni taarifa iliyotolewa na kampuni ya Ooredoo Mynmar ya nchini Qatar.
VIJIMAMBO

No comments:

Post a Comment