Pages

Friday, May 1, 2015

Snura amesema hatavaa nguo za nusu uchi tena kwakuwa ameshagundua makosa..

MWIGIZAJI wa kike na mwimbaji wa muziki wa Bongo Fleva, Snura Mushi ‘Majanga’, amesema hatavaa nguo za nusu uchi tena kwa kuwa ameshagundua makosa hayo.

Snura alisema awali alikuwa akivaa mavazi ya nusu uchi au nguo za kumbana, lakini kwa sasa amejirekebisha na anatambua nguo zinazompendeza ili kutokuleta sintofahamu kwa mashabiki wake.

“Kiukweli nashukuru ushauri wa watu katika suala la mavazi, nimeshajirekebisha kwa sasa sivai kama zamani mavazi yasiyofaa katika jamii,” alieleza Snura.

MTANZANIA

No comments:

Post a Comment