Pages

Friday, May 22, 2015

Vanessa Mdee amefiwa na dada yake mkubwa..

Muimbaji mahiri Vanessa Mdee amefiwa na dada yake mkubwa Anna Mdee, ambaye amefariki katika hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam,  jana Jumatano alfajiri. 

Anna ambaye alikuwa mfanya kazi wa kampuni ya sigara ya TCC na alikuwa katika kituo cha Dodoma kwa muda mrefu alikuwa India akipatiwa matibabu.

Anna na Vanessa ni watoto wa marehemu Sammy Mdee, aliyekuwa mwandishi mkongwe aliyewahi kuongoza gazeti la Daily News, Katibu wa Mwalimu Nyerere na pia mkurugenzi wa kituo cha AICC. Mazishi ya Anna yatakuwa Same Jumamosi saa 8 mchana.

Mungu Amlaze Pema Anna Mdee

MICHUZI

No comments:

Post a Comment