Pages

Friday, July 3, 2015

AMEMUUA MWENZAKE WAKIGOMBEA MWANAMKE WA BAA

WATU watatu wamekufa katika matukio matatu tofauti katika Wilaya za Tarime na Rorya akiwemo mtu aliyeuawa wakati wanagombania mwanamke.

Waliokufa ni Chacha Mwita (24) aliyechowa kisu kifuani na mwenzake wakigombea mwanamke wa baa huko Sirari. 

Kaimu Kamanda wa Polisi Tarime Rorya ACP Swetbert Njewike alisema kuwa matukio hayo matatu ya vifo yalitokea Julai mosi mwaka huu katika Wilaya za Rorya na Tarime.

Akielezea tukio la baa ambalo Mwita aliuawa, alisema siku hiyo marehemu akiwa baa moja katika mji wa Sirari, Tarime, nyakati za saa moja jioni kulitokea ugomvi kati ya marehemu na mtu mwingine ambaye hajafahamika jina lake wakigombania mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Dina.

“Jeshi la Polisi linafanya msako wa watuhumiwa wa mauaji Chacha Mwita na watuhumiwa waliohusika katika mauaji ya Nguka ili waweze kufikishwa katika vyombo vya Sheria,” alisema.

Aliwaonya wananchi kutojichukulia sheria mikononi ya kuwauawa watu wengine badala yake wawafikishe katika vyombo husika vikiwemo vya Dola. Aliwaomba raia wema kutoa taarifa mara watakapowaona watuhumiwa hao wa mauaji hayo ii wakamatwe.

HABARI LEO

No comments:

Post a Comment