Pages

Tuesday, July 14, 2015

Mzee Yusuph amesema lazima aache muziki

Mwimbaji mahiri wa muziki wa Taarab nchini ambaye pia ni mkurugenzi wa kundi la Jahazi Modern Taarabu, Mzee Yusuph amefunguka na kusema kuwa lazima aache muziki na kufanya kazi zingine nje ya muziki.

Mzee Yusuph alisema hayo alipohojiwa na mtangazaji wa Tam Tam za Mwambao ya East Africa Radio, Mwanne Othman.

Mzee Yusuph alisema kuwa kwa sasa anataraji kutoa album mbili za mwisho ili aweze kuachana na muzuki kwa swababu ana mambo mengi ya kufanya hasa siasa na kazi zake na badala yake atakuwa boss tu kwa wasanii wenzake katika kundi lake hilo ila si uimbaji tena.

"Muda ikifika nitaacha, lazima niache muziki kwa sababu nina mambo mengi ya kufanya nje ya muziki, na kama hivyo nikipita katika nafasi ya ubunge itabidi tu nicahgue moja itabidi kwenye muziki nisipatikane kwa asilimia mia moja vivyo wapenzi wa muziki wangu lazima waelewe kuwa naacha muziki kwa sababu ya siasa na kazi zangu zingine ambazo ni nyingi na zinahitaji uwepo wangu hivyo lazima niache muziki ili niweze kukamilisha mambo mengine nikiwa nje ya muziki."

Lakini mzee Yusuph aliweza kuweka wazi suala la yeye kutaka kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo la Fuweni Zanzibar na kusema kuwa anataka kulipa fadhila kwa namna ambavyo mashabiki wake walivyoweza kumpenda na kumjali na kuweza kumfanikishia mambo mengi kupitia njia ya muziki, hivyo yeye anaamini ubunge ni wito anaona bora awe mbunge ili jamii iweze kumtuma na kuwawakilisha wananchi katika mambo yao kwa kuwa wananch9o hao wameweza kumletea mabadiliko katika maisha yake ya kawaida.

Mbali na hilo Mzee Yusuph ameeleza kuwa yeye kuingia katika siasa si lengo ya kutafuta kutoka kimaisha bali anaamini anaweza kuwafanya jambo wananchi kwa kujitolea maana lengo lake ni kuwatumikia wananchi.

"Mimi sina ndugu sina baba ambaye ni kiongozi bali nimeingia katika siasa ili wananchi waweze kunituma maana mimi naamini hii kazi ni ya wito tu hivyo wananchi wasiangalie majina ya viongozi bali waangalie mtu mwenye dhamira njema ya kutaka kufanya jambo kwa manufaa ya wananchi na kwa kujitolea. Mimi naanzia kwenye ubunge ikiwezekana huko baadaye mpaka kwenye urais nitafika tu"


No comments:

Post a Comment