Pages

Tuesday, October 13, 2015

ASKARI AUAWA KWA KUCHOMWA KISU NA MTANGAZAJI WAKIMGOMBEA MSICHANA MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI BAA

Askari polisi wa mjini Babati, Mkoa wa Manyara ameuawa kwa kuchomwa kisu na mtangazaji mmoja wa redio kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.

Baadhi ya wakazi wa Babati walisema jana kuwa wanaume hao walikuwa wakimgombea mwanafunzi wa kidato cha pili walipokuwa baa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Christopher Fuime alimtaja aliyeuawa kuwa ni Rashid Haruna (30) mwenyeji wa Mkoa wa Njombe.

Kamanda Fuime alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 5.30 usiku eneo la Kitalu X.Alisema polisi wanamshikilia mwanafunzi huyo wakati uchunguzi zaidi kuhusu mauaji hayo ukiendelea.
Kamanda Fuime alisema baada ya mtangazaji huyo kumchoma kisu askari huyo alikimbilia sehemu za Dareda.“Kabla ya kifo chake alichomwa kisu mara 15 sehemu mbalimbali
za mwili wake ikiwamo mikononi, mgongoni, ubavuni na eneo la moyo,” alisema Kamanda Fuime.
Kamanda Fuime alisema mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda wilayani Makete Mkoa wa Njombe kwa maziko.Awali askari ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema siku ya tukio polisi huyo alimkuta msichana baa akiwa analumbana na mtangazaji. Alisema msichana huyo alimuomba askari ambaye ni mpenzi wake amsaidie kwani anang’ang’aniwa na mtu asiyempenda.
MWANANCHI

No comments:

Post a Comment