Pages

Saturday, October 10, 2015

Kali ya kampeni......Dovutwa kuunganisha elimu ya msingi na sekondari hadi darasa la 10, baada ya hapo ni chuo kikuu

CHAMA cha United People's Democratic Party (UPDP), juzi kimezindua kampeni za mgombea urais wa chama hicho, Fahmi Dovutwa, uliofanyika katika Viwanja vya Garden, Kilwa Kivinje, Wilaya ya Kilwa, mkoani Lindi.

Dovutwa alisema
"Katika sekta ya elimu nitaweka
mfumo ambao utaunganisha elimu ya msingi, sekondari. Mtoto atasoma hadi darasa la 10, baada ya hapo ataenda Chuo Kikuu, pia nitahakikisha mitaala inabadilishwa hasa kwenye elimu yamsingi ili kuinua kiwango cha elimu".

Katika mkutano huo, Dovutwa alimnadi mgombea ubunge wa Kilwa Kusini, kwa tiketi ya chama hicho, Fatuma Machalala na mgombea udiwani Kata ya Kivinje Singino, Ismail Namiwa.

MAJIRA

No comments:

Post a Comment