Pages

Monday, October 12, 2015

Sofa za kisasa sokoni kwa sasa ni za shape ya L



Kama kawaida yangu ya kupita sehemu mbalimbali ili kukuletea vitu vizuri kwa ajili ya nyumba yako leo nakuletea sofa za kisasa zilizopo sokoni. Sofa hizi ni zile zenye umbo la L. Sofa hizi zimependwa zaidi kwa sababu kadhaa:


Kwanza ni kuwa zinafiti vizuri kwenye kona ya sebule.

Pili, zinaruhusu nafasi kwa kuwa hizi haziwekwi kati kama ile seti ya sofa iliyozoeleka na wengi.

Tatu, kama una chumba kidogo unaweza kuitenganisha sofa ya umbo la L ukapata piece mbili.

Na nne ni kuwa sofa hii inajitosheleza kwa maana ya kuwa huhitaji kiti cha ziada sebuleni.

No comments:

Post a Comment