Pages

Sunday, October 4, 2015

Kingunge Mwiru ajitoa CCM....amesema hajiungi chama chochote ila anaunga mkono mabadiliko

Akizungumza kupitia vyombo vya habari Jumapili ya leo, mwanasiasa mkongwe katika Chama cha Mapinduzi (CCM) na aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali za chama na serikali ya Chama, Kingunge Ngombare Mwiru ametangaza rasmi hivi punde kujiengua uanachama ndani ya chama hicho.

Kingunge amesema ameamua kufanya hivyo kwa kuamini kuwa CCM haifanyi yale yaliyoasisiwa na kujengewa misingi bora na waasisi wa Chama. 
  
Aidha amesema hakusudii kujiunga na chama chochote cha siasa nchini. 

Akitathmimi anavyoiona hali ya sasa kisiasa nchini, amesema kila kundi katika jamii hivi sasa linataka mabadiliko. 


No comments:

Post a Comment