Pages

Saturday, January 2, 2016

HOME DECOR HAPA NA PALE.....KIOO CHA BAFUNI, MAWE YA KUKANYAGIA, MAKABATI YA JIKONI

Bila shaka hakuna ambaye hatapenda kioo na ukuta wa hili bafu. Mwaka huu nawe msomaji wangu uwe mzuri kwako kama bafu hili!
Nimependa idea ya kuweka hivi vimawe katikati ya haya mawe ya kukanyagia. Wapo wanaootesha majani huku kati badala ya hivi vimawe ila huwa inasumbua sana wakati wa kukatia kwani aidha inabidi gardener apinde mgongo kukata kwa mkasi ama abinue mawe yote ndipo apitishe mashine. 

Lakini vilevile majani kati  badala ya vimawe huwa yanafanya pattern nzuri sana kwa ajili kile kijani kinang'aa zaidi ya hivi vimawe. Sasa uamuzi ni wako wewe mwenye nyumba kuwa kipi ni kipi kutokana na faida na hasara ya kila moja. Wanasema kabla hujajenga mnara hesabu gharama.. 
Kabati za jikoni za mbao ya mninga au mkongo zinafaa zaidi ya nyingine zote. Sababu kuu ni uimara na ya pili ni tupende vya kwetu tunanyue uchumi wa nchi yetu.

Nishirikishe mapambo ya nyumba au bustani yako. Piga/whatsapp 0755 200023

No comments:

Post a Comment