Pages

Tuesday, January 5, 2016

VIVI MACHANGE HOMES.....CONSULTATION YANGU YA KWANZA KWA MWAKA HUU NI KWENYE HII NYUMBA



Niko excited na najiandaa kwa ajili ya hii project yangu ya kumshauri mteja wangu wa kwanza kwa mwaka huu. Nyumba ikikamilika mtapata taste ya nyumba zilizopokea ushauri wangu.

Inakuwaje? Ni kuwa mwenye nyumba anakuwa na jinsi anavyotaka nyumba yake iwe lakini kuna mambo hayaelewi, ninachofanya mimi ni kumsikiliza na kumshauri. Mara anaponilipa gharama za mwanzo ushauri wangu unaendelea hadi pale nyumba itakapokamilika. Gharama za pekee za nyongeza ni usafiri pale atakaponihitaji site au kwenda kununua fenicha na decorations.

Ushauri unaanzia wapi? Unaanzia popote kwenye stage yoyote ya nyumba kulingana na hitaji la mteja. Kuna mteja anataka aanze kushauriwa wakati wa wiring kama vile TV ikae upande gani, cooker na kadhalika. wakati kuna anayetaka kuanza kushauriwa kuanzia tiles na rangi...kwahivyo ni katika hatua yoyote ile kwa hitaji la mteja. Ulishawahi ona mtu anaweka fence na marembo mazuri lakini baadaye anakuja kuyaziba kwa makuti au vibati kwa kuwa anahitaji zaidi privacy? Pengine angepokea ushauri kabla angejenga kivingine.

Karibu sana...piga/whatsapp 0755 200023

No comments:

Post a Comment