Pages

Wednesday, January 6, 2016

VML:......Fahamu Top 10 ya Migahawa Jijini Dar es Salaam

Hii ni kwa mujibu wa  mtandao wa swahilicheftz.com....Kusema ukweli migahawa mizuri ni mingi ila kwa hii kwa mawazo yangu nadhani imeangalia mitaa ya uzunguni zaidi... Lakini naamini kama ulikuwa unafikiria mahali patulivu kwenda kupata msosi na rafiki au familia basi orodha hii itakusaidia sana kupata idea.


Wengi tunafahamu kula nje katika migahawa mbali mbali yaweza kua gharama na kwa wengine huchukuliwa kama stareh zilizo pitiliza.Migahwa hii 10 imeweza kufanya jambo la kula nje na kufurahia mapishi mbalimbali kua jambo la kuthaminiwa na kusherekewa na jamii nzima .Tutaanza na wa mwisho kuelekea wa kwanza ili kukupa orodha iliyokamilika .
Orodha imeandaliwa kwa uangalizi wa karibu zaidi wa team yetu ya takwimu .tukiangalia zaidi katika (customer engagement) mahusiano na wateja na (customer satisfaction ) yani kiwango cha kuridhika kwa mteja kulingana na gharama alizolipia. Karibuni!!

10.Epidor Tz
Kwa wale wapenzi wa mikate keki na bidhaaa tofauti za ngano mgahawa huu ulioko haile salasie masaki ni sehemu ya kufika epidor tz wamebobea katika ujuzi na ufananisi huo
520 Haile Selassie Rd |06 Shaaban Robert St | ☎️+255786669889 | |
ontact@epidor.co.tz | Dar Es Salaam |
9.samaki samaki fish n more;
Kwa wale wapenzi wa soka haswa ligi kuu ya uingereza wanaweza kua na ufahamu mkubwa wa mahala hapa haswa samaki samaki mlimani city mall hua inawapendelea sana wateja wake na mazingira mazuri ya kufurahia michuano hio na bila kusahau vibururdisho huduma nzuri na menu ya chakula iliyojitosheleza

8.Batman pizzeria
Pizza ni chakula chnye historia kubwa sana ya nchi ya Italy ,ukiwa Tanzania na unataka kupata pizza kama inayouzwa romaItaly ni vyema upite hapa !! cha kushangaza ni kua bei ni za kitanzania kabisa na sio za ulaya
Haile Selassie Road, Masaki. Pizza Hut

7.Bongo flava fast food :
Kwa wale watu wa kazi na wenye kupambana na foleni na pilika za Hi indo sehemu ya kwenda bongo fleva fast food ni wajuzi wa hali ya juu wa fast foods za aina mbali mbali hapa bongo haswa chipsi mayai chipsi kuku na kadhalika
Call 0655700312-Chole rd. Or 0758818317-Swahili street.

6.Capetown fishmarket dar
Wapenzi wa vyakula vya pwani haswa samaki (sea food) watakua wanapaelewa sana ! capetown fihmarket imeweza kubobea katika soko hili kwa kutoa huduma bora na madhari inayovutia sana ikiwa ufukweni na kusindikizwa na muziki wa live band

5.Ndoto polepole farm:
Kwa wale wapenzi wa safari za mbali na mji na kupata utulivu uku wakifurahia cakula kizuri na familia pamoja na wapendanao. Mahala hapa pana mandhari ya kuvutia sana pamoja na utulivu wa hali ya juu.Jambo lingine kuu na la msingi ni kuwa ndoto pole pole farm wameweza kufanya mazingira yao masafi nay a kupendeza sana pamoja na pool ya kisasa kwa wale wapendao kuogelea
Kerege, Dar Es Salaam, Tanzania

4.Terrace lounge :
Tukiongelea swala zima la vyakula vya nyumbani ukiwa nje hapa ndo mahala pa kwenda. Chakula kinachoandaliwa na terrace lounge ni sawa kabisa ama bora kidogo kuliko kile cha nyumbani.Terrace lounge inapatikana
Msasani citymall 3rd floor  .

3.Akemi dining:
Hapa ni habari ya mjini tukizingumzia mambo ya live music kutoka kwa mwanandada anetee ngongi akijulikana zaidi seghitodoll kwa ukurasa wake  wa instagram.Akemi imetokea kujulikana zaidi kwa business lunch haswa kwa wafanya biashara mbali mbali na wafanyakazi maofisini . jambo hilo limewezekana kwakuwa akemi ipo katikati ya jiji la dar es salaam nan i kivutio kikubwa sana kwa watalii wan njena wa ndani
Tanzania’s Revolving Restaurant & lounge 21st Floor, Golden Jubilee Towers, Ohio Street, Dar es Salaam.

2.Karambezi café
Hawa ni wajuzi wengine #1 wa vyakula vya pwani (seafood) mazingira na mandhari ya mahala hapa ni ya ufukweni kabisa ndani ya hoteli ya sea cliff dar es salaam tofauti ya karambezi café na sehemu ni nyingine ni utulivu na ufanisi wa hali ya juu ya wahudumu wake katika kuhakikisha mteja wao anapata huduma stahiki
With a 180 degree view over the Indian Ocean, we serve delicious SEAFOOD & INTERNATIONAL cuisine, in Sea Cliff Hotel in Dar es Salaam. KARIBU!

1.Cielo restaurante

Cielo ni mgahawa mpya kabisa jijini dar es salaam ambao unapatikana katika hoteli ya sea cliff village masaki cielo imeweza kua #1 katika orodha yetu kwakua ndio mgahawa ulioweza kujihusisha kwa karibu zaidi na wateja wake katika mitandao ya kijamii na pia katika hali halisi wakiwemo katika mahala husika hili ni jambo la migahawa mingi hapa mjini kujifunza

No comments:

Post a Comment