Pages

Monday, February 22, 2016

Fahamu aina za urembo wa kisasa wa nguzo za nyumba


Nguzo za nyumba ni sehemu ya fahari ya usanifu wa nyumba ambapo zinaweza kuwa ni kwa matumizi au ni kwa mapambo tu. Kuweka nguzo ndani na nje ya nyumba imekuwa ni njia mojawapi ya kufanya muonekano wa nyumba uvutie zaidi. Katika historia ya ujenzi, wahandisi na wasanifu wamekuwa wakibuni njia za kuongeza mvuto kwenye majengo. Nguzo zimekuwa zikitumika kuleta muonekano wa kifahari ndani na nje ya nyumba za kisasa na zinaweza kuwepo kwenye chumba chochote, japo zinapendeza zaidi kwenye
vyumba vikubwa kama vile sebule na jiko la wazi.

Zaidi ya kusaidia kubeba uzito wa nyumba hasa za ghorofa na kupeleka uzito sakafuni nguzo zina maumbo maarufu mawili ambayo ni pembenne na duara. Na hata kama zinakuwa na miferejji, reli au mabondemabonde lakini bado umbo kuu linabaki ni mojawapo kati ya haya mawili. Sasa basi ili nguzo zivutie machoni inabidi kuamua unazifunika na nini.

Zuberi Peter ambaye ni mrembaji wa nguzo anatuambia kutegemea na mtindo wa ndani ya nyumba yako, unatakiwa ufahamu ni urembo wa malighafi ipi ndio utafaa zaidi kwako. Kwamfano kama ndani ya nyumba kuna muonekano wa kiutamaduni, nguzo zilizorembwa kwa urembo wa kutengenezwa kwa saruji kali bila kuongezea mwingine ndio unaofaa zaidi.

Malighafi, ukubwa na mitindo mbalimbali inatumika kuweka urembo kwenye nguzo. Malighafi zinazotumika kwa nguzo za ndani ya nyumba ni pamoja na mawe ya asili ya granite, marble na mosaic.  Malighafi nyingine ni pamoja na plastiki, mbao, PVC, kioo cha nyuzi na chuma. PVC na plastiki ni urembo wa bei rahisi lakini unaleta muonekano mzuri sana na wa kifahari. Mbao zinatakiwa kwenye ngyuzo ambazo hazigusani na maji hata kidogo kwani zikishika maji zinapinda. Chuma zinatumika kuzungushia nje ya urembo.

Nguzo za kwenye varanda kwa ajili ziko mazingira ya nje zinapendeza zaidi zikirembwa kuendana na maringira hayo. Mfano, inaweza kutengenezewa urembo wenye kuonekana kama majani.


Kwa ushauri wa mapambo ya nyumba tuwasiliane 0755 200023

No comments:

Post a Comment