Pages

Sunday, February 21, 2016

VIVI MACHANGE HOMES: Project ya Kumshauri Mwenyenyumba Kuhusu Bustani za Kuzunguka Nje na Ndani ya Fence

Hey friends,
 Natumai jumapili inamalizika salama. Hii ni project yangu kwa sasa ambapo mteja anataka ushauri wa mitindo ya bustani za kuzunguka fence kwa nje na ndani. Habari ninayotaka ujue ni kwamba mteja wangu huyu yuko mkoani, kwahivyo huwa nafanya ushauri wa onsite na offsite. Kushauriana ni kuzuri wapenzi. Kama uko mbali nitakutumia picha nitakupa maelezo, tutajadiliana na utauliza lolote linalokutatiza na kwa muda wowote hadi upate unachokitaka. Na gharama yangu nakuchaji mara moja tu hadi kazi yako iishe..karibu
Hii ndio nyumba mwenye nayo anataka ushauri juu ya kuotesha bustani za kuzunguka hii fence kwa nje na kwa ndani. Uzuri wangu ni kuwa nakushauri, unaelewa nawe unakuwa mtaalam unaenda kufanya kazi yako mwenyewe kwa kumuelekeza kijana na bustani. Maana yake ni kwamba una save hela nyingi badala ya ungemuajiri landscaper/gardener...kwanini upoteze hela nyingi? Pata ujuzi kisha fanya mwenyewe!

Kwa ndani eneo la kona unaweza kutengeneza kitu kama hiki na ukaotesha kichaka chake cha maua, ukapata na kiukuta cha kukalia

kama kiukuta ni gharama basi tupia mawe na mimea namna hii.

Unaweza kuamua kuzungusha ukutani yale majani ya kutambaa, naamini ulishawahi kuyaona. Ukifanya hivyo kupiga ukuta  rangi tena ndio kwaheri.

Kwenye kona unaweza kuotesha maua mchanganyoko na eneo lingine ukaotesha boda ndefu.

Pia unaweza ukaacha udongo wazi kuonyesha mwisho wa ukoka kama hivi.

Ukiotesha hivi kwa nje inavutia.

No comments:

Post a Comment