Pages

Tuesday, February 16, 2016

PICHA: PATA IDEAS YA SEHEMU MBALIMBALI UNAZOWEZA KUWEKA VIKABATI VYEMBAMBA/SIDEBOARDS

Uki google neno sideboards utaona aina mbalimbali za hivi vikabati vyembamba.

Unaweza kuweka kikabati chembamba kwenye corridor endapo corridor yako ni pana. Zaidi ya mvuto pia kinakuongezea sehemu ya hukifadhia kwahivyo nyumba kuwa na mpangilio.
Vikabati vyembamba pia vinaweza kuwa bafuni chini ya sink na humo unahifadhia vitu mbalimbali kama vile tissue na dawa/sabuni za kusafishia.
Kikabati chembachmba pia unaweza kukiweka kwenye baa ya nyumbani. Kuna wenye nyumba ambao wana varanda zilizozibwa (aidha kwa grill) na pia wengine wana nyumba za ghorofa na wanapenda kuweka eneo la bar pale kwenye balcony. Kama unalo eneo kama hilo basi waweza weka kikabati chembamba/sideboard

Kikabati chembachea pia waweza kukiweka kwenye dining room. Juu ya kikabati panasaidia kama sehemu ya kuwekea mabakuli ya vyakula kabla ya kuanza ku serve na ndani unahifadhi vyombo vya kulia.

Kikabati chembamba kinapendeza kwenye chumba chochote, hapa sebuleni kimehusika kama kabati la TV

Je una tatizo lolote kuhusu mapambo ya nyumba yako? Nijulishe 0755 200023

Nifuate instagram: vivimachangehomes

No comments:

Post a Comment