Pages

Wednesday, November 16, 2016

Njia za kupamba meza ya chakula

Naomba ingia instagram @mtotomagazine u like picha hii hapa chini ili ishinde. Asante sana 

Tukubaliane kuwa hata kama ni ule wakati ambao meza ya chakula haitumiki sio sawa kujaa madaftari na vitabu vya kazi za shuleni ambazo huenda zilifanyikia hapo. Mara zote meza ya chakula inatakiwa kuwa katika muonekano wa kuvutia.

Ni rahisi kuandaa meza wakati wa
chakula ila kwa baadhi ni changamoto kuipamba baada ya chakula na wakati wote ambao haitumiki, kwani inawezekana unafikiria je, uweke pambo moja kubwa la kati au mstari wa vitu katikati ya meza, utepe au bila utepe na kadhalika.  Lengo ni kutengeneza muonekano wa kuvutia ambao utaendana na sehemu ya chumba iliyobaki na kutokuonyesha meza kuzidiwa na vitu!

Wakati unapokuwa umekaribisha watu nyumbani kwa chakula, ni rahisi kupendezesha meza kuendana na mandhari, rangi au hata majira ya tukio kama labda ni kipindi cha sikukuu fulani za mwaka. Yote haya yanakuruhusu kuipamba meza kwa staili yoyote unayotaka bila kujali kama itaendana na chumba cha chakula. Ila inapokuja ni swala la kupendezesha meza ya chakula kwa muonekano wa kila siku, ndipo tunaposema ni lazima mapambo unayotumia yaendane na muonekano wa chumba chote.

Kwahivyo kitu/pambo ambalo unatandaza juu ya meza yako mwaka mzima, inategemea na staili yako ya upambaji, na unaweza kutumia njia kadhaa kuipa meza yako muonekano wa kuvutia kila siku hasa wakati ambapo haitumiki.

Pambo moja kubwa katikati ya meza ni moja ya njia ya kuipendezesha ambayo imekuwa ikitumika tangu enzi. Kama hilo pambo ni refu unatakiwa kuhakikisha kuwa halishindani na ile taa ya kati ya kuning’inia juu ya meza (chandalia). Kama kitakuwa ni chumba cha chakula chenye taa mbili badala ya ile moja ya kati basi inawezekana kupamba meza kwa pambo lenye urefu kiasi.

Tumia trei la kila siku kama hauna pambo moja lenye ukubwa wa kutosha kuendana na ukubwa wa meza, tengeneza muonekano wa kitu kikubwa kwa kukusanya vidogo pamoja kwenye trei.

Njia nyingine ni kwa kutumia vitu viwili vilivyowekwa  katika mstari ulionyooka na umbali wa kulingana kutoka pale katikati ya meza inaponing’inia chandalia (hapa tunakisia kwamba meza yako ni ndefu kwahivyo itaruhusu muonekano huu).
Pia unaweza kutumia msururu wa vitu vidogo lakini vikawekwa kuendana na urefu wa meza. Hivi vitu kwa kawaida vinakuwa ni vidogo kwa maumbo zaidi ya ambacho kingeweza kikatumika peke yake ili kwamba visije kuizidi meza nguvu.

Utepe wa meza unaweza kuupamba kwa staili mbili ya kwanza ikiwa ni utepe pekeee na ya pili ni utepe na mapambo juu yake.

Tumia zile mati za kuwekea sahani hata kama sio wakati wa kuandaa chakula. Mati hizi zikiwa na rangi ya kuwaka zinapendeza na kugeuka kivutio cha meza. 


Haya sasa msomaji wangu niambie, kwa sasa umeweka nini juu ya meza yako ya chakula kwa lengo la kuipendezesha?

No comments:

Post a Comment