Mama yake #Beyonce, Tina KnowlesLawson (69) ameomba talaka kuvunja ndoa yake ya mara ya pili ili aachane na mumewe Richard Lawson (76).
Kwa mujibu wa nyaraka za kisheria zilizopatikana na mtandao wa TMZ, Tina ameanza mchakato wa kuomba talaka jumatano iliyopita.
Kwenye nyaraka hizo inaripotiwa Tina ameainisha sababu ya kutaka kuvunja ndoa ni tofauti zisizorekebisha pia ameomba baada ya talaka mahakama imrejeshee jina lake la mwanzo Celestine Knowles na pia kusiwe na matunzo ya mwenza (spousal support).
Ndoa ya Tina na Richard ina miaka 8, walioana 2015 ndoa iliyofanyika kwenye boti huko California na waalikwa wote walivalia white si baadhi yenu mnakumbuka mapichapicha eeh.
Mara ya kwanza Tina aliolewa na baba yake Beyonce, Mathew Knowles toka 1980 hadi 2011 na wakafanikiwa kuzaa mabinti wawili Beyonce na Solange.
Ndoa ya baba na mama Beyonce ilivunjika baada ya kugundulika Mathew wakati huo akiwa meneja wa kundi la kina Beyonce la Destiny's Child kazaa nje ya ndoa na muigizaji Alexandra White mtoto wa kiume anayeitwa Nixon Knowles aliyezaliwa 2010.
Awali Mathew alikataa Nixon sio mwanae lakini baadaye vipimo vya DNA ikathibitika ni mwanae.
Ndipo ndoa ya mama na baba Beyonce ikavunjika kwa mama Beyonce kuomba talaka na baada ya hapo kila mmoja akafunga ndoa mpya ambapo baba Beyonce alimuoa modo Gena Charmaine Avery toka 2013 hadi leo wako pamoja.
Wiki chache zilizopita Alexandra amehojiwa na jarida la Uingereza la the sun akasema mwanae Nixon hana ukaribu na dada zake (kina Beyonce na Solange) wala baba yake (Mathew Knowles).
Yani familia ya Knowles haitaki kujihusisha na Nixon.
No comments:
Post a Comment