Pages

Tuesday, July 25, 2023

HASIRA ZIMECHANGIA KUVUNJA NDOA YA DULLA MAKABILA



Kuhusu waliokua wanandoa #DullaMakabila na #Zaiylissa kuachana; Zaiylissa amefunguka " Nimemuacha kwasababu nimechoka, hajatulia na ana hasira sana".

Zaiylissa amesema ni kweli amepewa talaka 3 kwa mpigo ambazo Dulla aliziweka kwenye bahasha na zikawasilishwa nyumbani kwa Zaiy Chamanzi.

Akielezea maisha ya ndoa kwa miezi miwili na siku 10 alizoishi na Dulla; Zaiy amesema Dulla alikua na matukia ya rejarejaja yasiyo na kikomo ikiwemo kumfumania na meseji za warembo wa mjini na akimhoji anaambulia kipigo.

" Sio rahisi kuishi na Dulla kwa ajili ana kashkashi nyingi na hata wakati naolewa baadhi ya ndugu zake waliniita pembeni na kunisihi Dulla hajatulia niwe naye makini", ameeleza Zaiylissa, akaendelea kusema kuwa amejitahidi sana lakini uvumilivu umemshinda ameamua kuchapa lapa na kusepa.

Zaiylissa akaendelea kufunguka kuwa tokea awe kwenye mahusiano na Makabila hakuwahi kuchepuka hali ambayo hadi mume alimuuliza mbona huchiti maana kila akipekua simu hakutani na sintohamu yoyote.

Zaiylissa akamalizia maelezo yake kwa kusema kingine kilichofanya ndoa na Makabila imshinde ni kwamba Dulla ana hasira sana ambazo mara zote ziliishia mwilini mwa Zaiy kwa kipigo.

No comments:

Post a Comment