Nyota wa muziki wa Singeli Tanzania mwanamuziki Dulla Makabila amekiri kuwa ndoa yake na muigizaji wa tamthilia ya juakali Zaiylissa imevunjika.
Tetesi za kuvunjika ndoa hiyo zilianza mwanzoni mwa wiki iliyopita baada ya mkewe kuondoa picha zao zote za pamoja na kumu unfollow mumewe kwenye account ya instagram.
Leo julai 24, 2023 Dulla akihojiwa na kipindi cha radio kwa njia ya simu amekiri ni kweli ndoa hiyo imevunjika.
Aidha kuna picha na video zinazomuonyesha Zaiylissa akiwa na vidonda vibichi vinavyochuruzika damu ikiaminiwa vimetokana na kipigo toka kwa ex wake.
Dulla na Zaiylissa walifunga ndoa may 12. 2023.
Ndoa ambayo imedumu kwa miezi miwili.
Miaka ya nyuma wote walishafunga ndoa na wapenzi wengine ambazo nazo zilivunjika.
Kwa Matangazo wasiliana na 0755200023.
No comments:
Post a Comment