Pages

Wednesday, February 4, 2015

Mmhh hawa wanawake wamefikiria sana, wanapasua kupe mkubwa anamwaga damu hivyo kumaanisha tohara imefanyika

kupe mkubwa
WANAWAKE wa Kimasai wanaopinga suala la tohara kwa watoto wamegundua njia nyingine ya kukabiliana na ukeketaji kwa kutumia kupe wakubwa.

Hayo yalielezwa katika warsha ya kujipanga kupokea mradi wa kijiji cha dijitali, iliyofanyika katika kijiji cha Ololosokwan hivi karibuni.

Wakijadili changamoto ya ukeketaji kama sehemu ya shida kubwa ya jamii kiafya, wanawake wamesema kwamba hukamata kupe wakubwa na kuwaua kisha kupiga vigelegele kuonesha kwamba mabinti wao wamepewa tohara.

Mmoja wa washiriki wa warsha hiyo alipouliza inakuwaje hapo baadaye binti anapokuwa mkubwa, aliambiwa kwamba ni rahisi kwa binti huyo hapo baadae kuzungumza na mwenzake wakaelewana.
“Tatizo la tohara ni la wanaume, wanaume hawa ndio wanahimiza wanawake wawe na tohara kwa kuwa wanataka kuwaoa wanawake ambao wameingia tohara kama wao,” alisema mama mmoja.


Alisema namna hiyo imefanya kuwakwepesha mabinti wengi na vurugu za tohara, ambazo kiafya si sawa, hasa kutokana na tatizo linaloambatana na kovu wakati wa uzazi na pia kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa upande wa mwanamke.

No comments:

Post a Comment