Pages

Monday, March 9, 2015

MENEJA: UJAUZITO ULIMKOSESHA SNURA MAMILIONI YA PESA

Wakati msanii wa Bongo Fleva,Snura Mushi yuko kimya kwa zaidi ya miezi kwa karibu miezi mitano na zaidi ili kupisha ujauzito wake ukue kwa siri hadi akajifungua mtoto wake wa tatu
zaidi ya mwezi mmoja uliopita, Snura ijumaa iliyopita aliachia ngoma yake mpya iitwayo ‘Hawashi’ na kuifichua siri yake ya kubeba ujauzito na kuficha siri hadi anajifungua.

Kwa mujibu wa meneja wa msanii huyo aitwaye HK Hyper, alisema kuwa kipindi hicho wakati Snura akiwa mjamzito alikuwa akipigiwa simu mbalimbali za kufanya shoo na kwamba wamekosa pesa nyingi sana.

“Kiukweli nilikuwa nikipigiwa simu nyingi sana za shoo lakini kutokana na ujauzito wake ilishindikana kwenda kwenye shoo hizo na tumekosa mamilioni ya pesa kwa kipindi hicho lakini tangu amejifungua amefanya shoo zaidi ya tatu” alisema HK.


Chanzo: Clouds fm

No comments:

Post a Comment