Pages

Thursday, April 9, 2015

Kanye West Aomba Msamaha kwa Kosa la Kumpiga Paparazzi


Kanye West ametekeleza matakwa ya kesi iliyokuwa ikimkabilia ya kumpiga paparazi.

Paparazi huyo alimtaka West kukutana naye palepale alipompiga na
kumuomba msamaha na kisha salamu.

Sasa picha zimeibuka zikionesha mwanamuziki huyo wa mdundo wa kufoka akitabasamu na paparazi aliyemshtaki.

Mpiga picha wa magazeti ya umbea Daniel Ramos alimshtaki West kwa kumshambulia baada ya kumuuliza kwanini alikuwa anasusia maswali ya waandishi wa habari nje ya uwanja wa Los Angeles..
Wakili wake ,Gloria Allred amesema kuwa wawili hao walikutana na West akaomba msamaha.

Kanye West ametekeleza matakwa ya kesi iliyokuwa ikimkabilia ya kumpiga paparazi.

Hata hivyo vipengee mahsusi ya makubaliano hayo na msamaha hayajabainika.

Kwa upande wake wakili anayemwakilisha bwana West ,Shawn Holley, amenyamaza kimya!
West, 37, aliomba mahakama imuonee huruma kwa kosa hilo la kumvamia mtu.

West anachunguzwa.
BBC

No comments:

Post a Comment