Pages

Wednesday, April 22, 2015

VAZI LA TAIFA LITAKALOWATAMBULISHA WATANZANIA POPOTE PALE WALIPO DUNIANI LITATANGAZWA HIVI KARIBUNI

Serikali  imesema wakati wowote kuanzia sasa itatangaza vazi la Taifa litakalowatambulisha Watanzania mahali popote walipo duniani.

Akizungumza na
NIPASHE jana, Afisa Habari katika  Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Concilia Niyibitanga, alisema, hadi sasa serikali imeshakamilisha mchakato wake baada ya kupitishwa kwa mapendekezo ya sampuli mbili ya vazi la kitenge na kanga.

Kwa mujibu wa Concilia, baada ya mchakato huo kukamilika, kinachosubiriwa ni kwa Waziri wa wizara hiyo, Dk. Fenela Mukangara (pichani), kulitangaza rasmi kwa umma muda wowote kuanzia sasa. Alisema, vazi hilo lingeshatangazwa muda mrefu, lakini majukumu ya kiserikali ndiyo yaliyofanya tangazo hilo  kuchelewa kutolewa.

“Mchakato umeshakamilika, serikali imemaliza kazi yake kwani ndiyo iliyokuwa inasubiriwa. Kuna mapendekezo ya sampuli mbili za kanga na sampuli mbili za kitenge.  Lingeshatangazwa, lakini kutokana na Waziri kubanwa na majukumu ya kiserikali ndiyo maana kazi imefikia hapa,” alisema na kuongeza:


“Waziri atalitangaza vazi hilo kwa umma muda wowote kuanzia sasa. Kwa sasa anakabiliwa na majukumu ya maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge… baada ya kazi hiyo atatangaza, maana watu wengi wanauliulizia.

No comments:

Post a Comment