Pages

Friday, May 15, 2015

Aina hii ya kitanda inakufaa wewe mzazi mwenye vyumba vidogo vya kulala

Msomaji wangu kama unaona ninachokiona utakubaliana na mimi kuwa kitanda hiki kinafaa mno kama chumba cha mwanao ni kidogo. Hapa watoto wanajipatia eneo la kompyuta/kusomea pamoja na droo za kuhifadhia. Na pale ambapo mvungu ungetumika bure kuna kitanda kingine kwa chini ambapo mtoto mwingine anatumia badala ya wote wawili kulala kitanda kimoja. Watoto kulala chumba kimoja ni jambo jema kwa ajili ya kujenga ile bondi ya udugu. Huu ubunifu ni mzuri.
Picha hisani ya instagram:fancyhomedecor

No comments:

Post a Comment