Pages

Wednesday, May 6, 2015

Mvua zitakoma mwisho wa mwezi huu

MVUA za masika zinazoendelea kunyesha zinatarajiwa kukatika mwishoni mwa mwezi huu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Hali ya Hewa
(TMA), Dk Agnes Kijazi alisema hayo alipokuwa akizungumzia mvua zinazoendelea kunyesha Dar es Salaam na maeneo mengine ya nchi.

Alisema ndani ya msimu huu wa mvua kutakuwa na vipindi vifupi vya mvua nyingi.

“Mfano mvua zilizonyesha Zanzibar zimenyesha kwa muda mfupi, lakini kwa wingi hadi kuleta mafuriko.“Zanzibar mafuriko yaliyotokea juzi saa tatu asubuhi kituo cha mamlaka kilipima milimita 196.1. Mei tatu mwaka huu ilinyesha masaa machache kituo kilipima milimita 172.2. Hii ndiyo ilileta mafuriko,” alisema Dk Kijazi.

Alitoa angalizo wananchi wajitahidi kufuatilia taarifa zinazotolewa na mamlaka hiyo ili kuepuka kupata matatizo.

HABARI LEO

No comments:

Post a Comment