Pages

Wednesday, May 6, 2015

Wabunge wamtimua tena Nyalandu....Bajeti hatarini kutopitishwa

Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii iko hatarini kutopitishwa, baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kukataa kwa mara pili kuijadili.

Wabunge wa Kamati hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wake, James Lembeli,
walifikia uamuzi wa kutoijadili tena na kuwaamuru viongozi wa Wizara hiyo wakiongozwa na Waziri Lazaro Nyalandu (pichani), kurudi tena baada ya wiki moja wakiwa wametekeleza maagizo yaliyotolewa na kamati.

 Maagizo hayo ni pamoja na kukaidi amri ya Mahakama Kuu ya kukataa kuanza mara moja utekelezaji wa tozo mpya kwenye Hifadhi za Taifa.

Lingine ni utaratibu wa kiingilio kwenye hifadhi na kwamba tozo iliyotakiwa ni kila mtalii anapoingia anapoingia anatozwa kiingilio na akitoka na kutaka kuingia tena ni lazima alipe.

Agizo lingine ni mgogoro wa mipaka kwenye Hifadhi ya Taifa ya Saadani. Kamati iliagiza kuwa mipaka ya hifadhi hiyo ibaki kama ilivyokuwa tangu awali, lakini kinyume chake, wizara imemega sehemu ya ardhi na kuitafutia hati miliki.

Kutokana na maagizo hayo, Kamati hiyo juzi iliwaagiza viongozi hao wa Wizara ya Maliasili na Utalii kufika katika kamati hiyo jana wakiwa na maelezo yote.

Licha ya maagizo hayo, viongozi wa Wizara hiyo walipofika katika Kamati hiyo jana hawakuwa wametekeleza maagizo hayo, hivyo waliamliwa kurudi  Mei 14 mjini Dodoma wakiwa na maelezo kamili.

Akitoa sababu za kushindwa kuwasilishwa na kutekeleza maagizo hao, Waziri Nyarandu alieleza kuwa muda wa siku moja waliopewa na Kamati ni mdogo kutekeleza maagizo yote.

NIPASHE

No comments:

Post a Comment