Pages

Friday, January 8, 2016

KANUNI 5 ZA NAMNA YA KUTUNDIKA PICHA ZA UKUTANI

Kutundika picha ukutani ni sanaa kama zilivyo sanaa nyingine. Muhimu  ni kubalance nafasi, rangi na ukubwa wa fremu
1. Inashauriwa picha/fremu ziwe kwenye level moja
2. Picha zitundikwe usawa wa jicho hasa pale ukuta hauna kizuizi ( fenicha) ila endapo kuna fenicha basi tundika mara tu baada yake na kama fenicha hiyo ni sofa zingatia picha zisigusane na kichwa cha mkaaji kwani zitamkera.

 Pia kwenye picha hii tunaona kuwa kwenye ubunifu unaweza kuvunja kanuni. Kwa mfano huyu katwist kidogo na kuvunja kanuni ya level lakini bado imependeza. Nadhani cha muhimu hapa ni kuwa kunyoosha yaani picha hazijapinda.
3. Hakikisha kuna balance na uwiano wa ukubwa wa picha. Unaona jinsi kubwa na ndogo zilivyochanganywa lakini bado zimevitua
4. Usitawanye picha ukuta mzima. Weka eneo moja kutengeneza focal point na umbali kati  ya picha na picha hasa zile zinazolingana inashauriwa uwe sawa.Kama ni kubwa zaidi basi ongeza umbali mara 2.
5. Inashauriwa kupanga picha sakafuni kwanza kuona jinsi zitakavyoonekana ukutani hasa zile zinazoelezea tukio yaani zilizoko kwenye sequence. Au pia kuna zenye maua ambayo yako vipandevipande kwamba lazima uziweke kwenye mpangilio fulani ili zifanye ua kamili.
Nawe msomaji wangu nishirikishe jinsi ulivyotundika picha zako za ukutani. 

No comments:

Post a Comment