Pages

Monday, January 18, 2016

KUTOKA KWA MDAU:..Eneo Nililojenga Maji Chini ni Mengi, Rangi Inabanduka.... Nimeamua Kuweka Tiles

Mdau wa VML anatuambia stori yake kutokana na kuwa eneo alilojenga lina maji mengi chini, kwahivyo inasababisha rangi inabanduka kwenye ukuta. Alichoamua kufanya ni kufuata ushauri aliopewa wa kitaalam wa kuondoa rangi yote na kuanza upya. Twende naye tuone anachosema:
Rangi yote nimekwangua. Ukuta nusu ya chini naweka tiles za decorations za ukuta wa nje na eneo la juu ndio nitapaka rangi.
Hii ni fence ya ukuta kwa ndani. Hilo jiwe kubwa hapo naweka fontain (maji yanayoporomoka)
Kotekote nimekwangua rangi hadi getini.
Muonekano wa chini wenye tiles umeshaanza kuonekana. Nguzo nimezipamba kwa mosaic.
Ukuta wa fence kwa nje.

Ama kweli nyumba yaweza kukuingiza gharama mara mbili mbili.
Nawe msomaji wako nasubiri stori yako ya mapambo ya nyumbani kwako. Ukishea ujuzi unajisikia vizuri. Piga/whatsapp 0755 200023. Asante

No comments:

Post a Comment