Pages

Monday, January 11, 2016

VML:...REUSABLE ICE CUBES HAZITAYEYUSHA KINYWAJI CHAKO NA KUKIPUNGUZIA LADHA

Ni kweli kuwa kuna watu wengi tu hawapendi vipande vya barafu vya kawaida kwani vinayeyukia kwenye vinywaji vyao na kufanya ladha iwe dhaifu kuliko ambavyo ingetakiwa iwe.. Habari njema ni kwamba kuna
mbadala ambao ni vipande vya barafu za kutumia zaidi ya mara moja.
Vipande vya barafu vinavyotumika zaidi ya mara moja (reusable ice cubes) ni vidude ambavyo vimetengenezwa kwa malighafi tofautitofauti ila vingi vikiwa ni vya plastiki, ambapo ndani yake kimewekwa maji safi ya kudumu ambayo ndio yanaganda kwa ajili ya kufanya barafu.

Barafu za kutumia zaidi ya mara moja zipo za miundo mbalimbali na yakuvutia kwa mfano pembe nne, samaki, vipande vya matunda na mingine mingi cha muhimu tu ni kwamba vyote hivyo vinagandishwa na kutengeneza barafu. Pia rangi zake zaweza kuwa bluu, njano na nyeupe.

Barafu hizi ni sahihi kwa wale ambao hawana haraka na vinywaji vyao. Hii ni kwasababu haziyeyuki haraka kwani barafu iko ndani lakini nje ni plastiki. Barafu hizi pia ni muhimu kama ifuatavyo:

Zinafanya kinywaji kuwa baridi bila kuyeyukia ndani yake. Hazifanyi kinywaji chako kipoteze ladha. Hii ni kwakuwa hakuna maji yanayoingia kujichanganya kwenye kinywaji chako kama zile barafu nyingine za kawaida ambazo zinayeyukia ndani na hivyo kuondoa ladha halisi. Na wengi wanapenda vinywaji vya baridi ila inaonekana kuwa wanachukia vipande vya barafu vya maji kwani vinayeyukia ndani ya kinywaji na kukipunguzia ladha yake ya mwanzo.Kama wewe ni mmoja wao basi tumia reusable ice cubes.

Barafu hizi unaweza kuzitumia tena na tena, unachotakiwa tu ni kuwa baada ya kutumika  zioshe, zifute na kuzigandisha tena. Zihifadhi kwenye friza kwa ajili ya kutumia wakati wowote.

Barafu za kutumia zaidi ya mara moja nyingi ni za plastiki au malighafi nyingine na ni za kutengeneza kiwandani ambapo zinaonekana kama barafu za maji yaliyoganda (za siku zote zilizozoeleka ziadi) ila ndani yake kuna maji ambapo unaweka  kwenye friza na ndipo hayo maji ya ndani yanaganda. 
Umuhimu wake hapa ni kuwa na matumizi mazuri ya maji, yaani huna haja ya kujaza maji kugandisha barafu kwani maji ya kudumu yako kwenye hivi vidude tayari.

Na licha ya haya matumizi mazuri ya maji bado wakati mwingine huna uhakika juu ya usalama wa maji yaliyotengengenea barafu za kawaida kama hukuyaweka mwenyewe.

Barafu hizi ni za kudumu. Endapo hivi vidude havitapasuka maji yake ya ndani yapotee basi unaweza kuvitumia maisha yako yote na hata vizazi vya mbele yako.

Barafu za kutumia zaidi ya mara moja zinasaidia kukifanya kinywaji kiwe baridi kwa asilimia 20 zaidi ya barafu za kawaida.

Kama bado huna nenda kanunue, zinauzwa madukani. Ni nzuri sana kwa nyumbani na kwenye sherehe.


Na kama ulikuwa hujui basi ukialikwa kwenye kimnuso ukakutana na hivyo vidude, fahamu ni reusable ice cubes kwa hivyo chota upooze kinywaji chako.

Nawe msomaji nishirikishe uvumbuzi wowote uujuao kuhusu maisha yako ya kila siku hapo nyumbani kwako. Ukishea ujuzi unajisikia vizuri. Piga/Whatsapp 0755 200023

No comments:

Post a Comment