Pages

Wednesday, March 30, 2016

TEMBELEA LINK YA VINAVYOUZWA..

Wapenzi, zaidi ya kukinga meza isikwaruzwe na  vyombo, table mats pia zinapendezesha maandalizi ya meza kwa chakula. Kuzinunua pamoja na bidhaa nyingine nyingi tembelea link ya vinavyouzwa hapo juu. Asante


Tuesday, March 29, 2016

Kanuni 10 za mpangilio wa sebule

Iwe ni chumba kitupu yaani sebule mpya au ni ya zamani lakini unataka muonekano mwingine, kupanga fenicha sebuleni inaweza kuwa ni changamoto. Unachotakiwa kufanya ni kufuata hatua hizi zenye kanuni za mantiki na ndipo utagundua kwamba kumbe mpangilio huo ni jambo rahisi tu.

Chagua eneo la kivutio cha chumba
Kamwe usidharau nguvu ya eneo macho yanapoelekea mara wewe au mgeni wako aingiapo sebuleni. Kuna wakati eneo hili linajitengeneza lenyewe kwa mfano eneo lenye dirisha kubwa au usanifu mwingine wowote uliofanyika wakati wa ujenzi. Vinginevyo unaweza kulitengeneza kwa mfano eneo ambalo luninga na miziki itakaa. Popote pale penye eneo hili la kivutio ndipo unatakiwa upange fenicha kupazunguka.


Usigusishe fenicha na ukuta
Ukubwa wa chumba ndio unaamua ni eneo kiasi gani libaki ukutani bila kugusana na fenicha, ingawa hata kwenye sebule ndogo kabisa unapaswa kuacha

Monday, March 28, 2016

Jinsi ya kutumia rangi ya kijivu kupendezesha nyumba yako

Kwa wengi tumezoea kuona rangi ya kijivu ikiwa imepakwa kwenye maeneo kama kuta za viwandani, mahospitalini, shuleni na zile sehemu nyingi ambazo kuzipendezesha sio muhimu. Wengi hawafikirii kuwa rangi hii inaweza kupambwa nyumbani na ikavutia sana. Kijivu mara nyingi inaendana na mazingira na kuna njia nyingi unazoweza ukaitumia kupendezesha nyumba bila kuzidisha au kuigeuza kama eneo lililofifia. Vilevile kijivu

Mambo ya kuzingatia unaponunua shuka


Shuka zinachukua nafasi kubwa ya kuwa kivutio cha kitanda. Unapoamua kuzinunua kuna mambo kadhaa ya kuzingatia. Mara nyingi wanunuzi wanaangalia rangi, michoro, ukubwa na bei. Hata hivyo vitu hivi  pekee havitoshi kuthibitisha ubora wa shuka hizo unazotaka kununua.

Kuchagua kitambaa cha shuka chenye ubora wa hali ya juu ndio jambo muhimu zaidi. Kwa kuzingatia hili zifuatazo ni

Saturday, March 26, 2016

HERI YA PASAKA WAPENZI!

Nimetumia hii picha ya taa ya mezani kukutakia heri ya pasaka kwa ajili nataka tujifunze jambo. Tunaponunua taa za mezani tuangalie muundo na sanaa zilizobeba. Kwa mfano hii yenye kitako cha jogoo, bila shaka itamvutia yeyote atakayefika nyumbani kwako. Sikukuu njema kwako!

Tuesday, March 22, 2016

Faida za kumhusisha mtaalam kufremu picha unazotaka kutundika ukutani

Huenda ndio umetoka fungate na umepokea picha zako za harusi, kwahivyo wewe na mume wako mnaanza kufikiria na kuchambua ambazo mngependa kukuza na kutundika ukutani. Au labda umepata mtoto na ni wakati wa kumuongeza kwenye hazina ya picha za familia ulizotundika ukutani. Vyovyote vile, kufremu picha ni sanaa inayohitaji msanii anayeijua vizuri kazi hiyo.

Fremu za picha iwe ni za mbao, plastiki au chuma huwa zinahusisha miundo ambayo picha inapowekwa ndani yake inaruhusu kuwa kivutio kwa wale wanaoitazama. Fremu yenyewe tu ni sanaa ambapo utakapochagua ya rangi na muundo sahihi bila shaka inajisimamia yenyewe kabla hata haijawa na picha ya ndani!

Ingawa ni ukweli kwamba wapo watu wanaonunua fremu na kuweka picha peke yao, ni vyema kufahamu kuwa msanii wa picha na fremu ana uzoefu na utaalam wa kujua ni fremu ipi inafaa kwa picha ipi. Na pia anajua hatua sahihi za kupitia ili kufremu picha katika ubora unaokubalika. Fikiria thamani ya picha zako kwa

Vigezo vya pazia za chumba cha kulala



Katika chumba chochote ndani ya nyumba, pazia linachukua sehemu kubwa ya muonekano kwa kivyo linaweza kuwa kivutio au likaharibu. Habari njema ni kwamba kuna aina nyingi za mitindo ya mapazia kuendana na kila nyumba na kila gharama. Yapo mapazia ya kifahari sana na yapo ya gharama nafuu kabisa.

Ili kupata matokeo unayoyataka, kuna baadhi ya

Monday, March 21, 2016

Zingatia haya unapojiuliza uchague kitambaa cha sofa chenye michoro au cha rangi moja.

 
Kuna vingi vya kuchagua pale ambapo unaamua  kupamba nyumba yako kwa jinsi unayotaka wewe.  Aina na mitindo mbalimbali ya fenicha, pazia na mazulia zipo sokoni za kumfaa kila mmoja na vivyo hivyo kwa vitambaa vya sofa.

Baada ya kusema hayo, kutokana na kuwa na machaguo mengi inaweza kukuwia vigumu kuchagua kitambaa sahihi cha sofa kwa ajili ya

Thursday, March 17, 2016

Hatua sahihi za kusafisha meza ya kioo

Meza ya kioo inaweza kutumika kwenye nyumba yako katika vyumba ambavyo ni pamoja na sebuleni, chumba cha chakula na hata chumba cha kulala. Wapo wanaozitumia kwenye varanda na bustanini pia.  Bila kujali ni wapi ilipo meza yako ya kioo, ni wajibu wako kuhakikisha kuwa ipo katika hali nzuri kwa kuisafisha kwa kina kila inapochafuka.

Meza safi ya kioo ni pale inapokuwa na kioo kinachong’aa bila uchafu wowote. Vifaa unavyohitaji kusafishia ni dawa ya kusafishia vioo au maji mepesi kwa maana ya yasiyo na chumvi kwani huwa chumvichumvi zinaacha alama kwenye kioo, kitambaa kikavu na gazeti.

Fuata hatua hizi za jinsi ya kusafisha meza ya kioo ili ionekane kama mpya kila wakati.

1.     Hatua ya kwanza katika kusafisha meza ya kioo ni kuondoa kila kitu juu ya meza. Viweke pembeni na ukishamakiza kusafisha utavirejesha.

Tuesday, March 15, 2016

Namna ya kuweka mpangilio kwenye kabati la nguo


Kabati la nguo kwenze chumba cha kulala ni fenicha muhimu. Ingawa linajulikana kama kabati la nguo, linahifadhia vitu vingi mbali na nguo. Vitu hivyo ni pamoja na nguo zenyewe, viatu, masanduku, mabegi, vitupio vya urembo na vitu vingine vingi ndani za chumba chako hicho hivyo kukuwezesha kuwa na mpangilio wa vitu chumbani.

Kuna miundo miwili mikuu ya milango ya makabati ya nguo ambayo kutokana nayo unaweza kuongeza au kupunguza maeneo ya kuhifadhia. Makabati ya nguo yenye milango ya kufungua kwa kutelezesha ni mazuri pale ambapo chumba ni kidogo na hakuna eneo kubwa kuruhusu milango ya kufunguka kwa nje.  Wewe mwenye chumba cha hivi utafurahia zaidi kabati lenye milango ya muundo huu kwani utabakiwa na eneo kubwa chumbani. Kwa muundo wa pili wa makabati yenye milango ya kufunguka kwa nje yanakupa wigo mpana zaidi wa eneo la kuhifadhia ndani ya kabati hilo. Cha msingi kwa aina hii ya kabati ni chumba kuwa na nafasi ya kutosha kuruhusu milango kufunguka kwa nje na bado wewe au mwingine akaweza kupita na kupishana vizuri  kwa uhuru chumbani.

Kimsingi pangilia ndani ya kabati lako la nguo kama ifuatavyo:

·        Kwakuwa ndani ya kabati kuna vyumba/maeneo mbalimbali kama vile mashelfu ya juu na chini, madroo, fimbo ya kutundikia nguo na kulabu za kuning’iniza vitu. Kwenye shelfu za chini utahifadhia viatu endapo hujatundika mfuko wa viatu mlangoni mwa kabati hala pale milango ya kabati inapokuwa ni ile ya kufungua kwa kutelezesha. Tumia mashelfu ya juu kuhifadhia masanduku, mabegi na vile vitu ambavyo havitumiki mara kwa mara.

·        Jitahidi kutumia henga zinazofanana kwenye nguo zote ulizotundika. Lengo kuu ni matumizi sahihi ya nafasi na kufanya mpangilio uvutie.
·        Kama hazipo, weka kulabu (hooks) kwenye milango ya kabati kwa ajili ya kutundika mikanda, kofia, tai, skafu na mikoba. Hii ni kwa yale makabati yenye milango ya kufunguka kwa nje.
·        Panga nguo ndani ya kabati kwa makundi: Kundi la blauzi, jaketi, sweta, makoti,shati, suruali, suti, sketi, gauni, kaptula, fulana na kadhalika.
·        Tumia droo ndogo kuhifadhia soksi na nguo za ndani.

Kwa mpangilio huu hakika utalifurahia kabati lako la nguo kwani licha ya kuvutia ni kwamba litakurahisishia kupata kwa haraka na wepesi kile unachohitaji ndani ya kabati.


Vivi anakuwezesha kupendezesha nyumba yako. Simu 0755200023

Monday, March 14, 2016

Jinsi ya kuchagua muundo wa ngazi za nyumba

Ngazi ni eneo muhimu la nyumba ambalo linawasaidia wakaaji wa nyumba hiyo kwenda maeneo mengine ndani ya nyumba husika, hasa pale nyumba inapokuwa ni ya ghorofa. Mbali na hilo, muundo wa ngazi pia unahusika kwenye kupendezesha nyumba.

Mhandisi David Sembuyagi anasema kuna aina nyingi za ngazi. Ngazi ni gharama na pia ni ngumu kuzijenga. Kwahivyo ni muhimu ukafahamu hayo wakati unapochagua muundo wa ngazi. Kama upo kwenye mchakato wa kujenga nyumba itakayohusisha ngazi basi makala haya yatakusaidia kuamua muundo wa ngazi ambao utakufaa. Dondoo hizi zitakufanya uje na uamuzi wenye uzito:

1.      Bajeti
Miundo mbalimbali ya ngazi ina gharama tofauti. Bajeti yako itaamua mtindo, muundo na malighafi ya kutengenezea ngazi zako.

2.      Nafasi
Nafasi iliyopo ndani ya nyumba inayohusika kwa ajili ya kuweka ngazi inatakiwa kuangaliwa kwani ndio inaamua muundo wa ngazi utakaofaa. Kama nyumba ni ndogo, ni vyema kuchagua muundo wa ngazi ambao hautachukua nafasi kubwa. Na kwa upande mwingine kama nafasi ni kubwa basi unaweza kuchagua ngazi ya muundo wa kuvutia na kubwa, au pia unaweza unaweka mbili upande huu na ule.

3.      Usalama
Kwenye usalama wa ngazi ni lazima kuzingatia mlalo na mwinuko wa hatua usiwe mkali, na pia kizuizi cha pembeni ni muhimu hasa ngazi inapokuwa ni ndefu na ni lazima kwa ngazi ya kupanda ghorofani.  Usalama wa ngazi pia uzingatie uwepo wa watoto na wazee ndani ya nyumba. Upana uwe wa kutosha kuweza kupishana watu wawili,  anayeshuka na anayepanda.

4.      Malighafi
Malighafi kwa ajili ya kutengenezea ngazi zipo za aina kadhaa. Mwenye nyumba anaweza kuchagua ngazi ya malighafi ya chuma, mbao au tofali kwa ajili ya nyumba za kisasa. Kinachotakiwa ni kuhakikisha kuwa malighafi zinazochaguliwa zitaendana na muonekano mzima wa nyumba, ubora uzingatiwe kwani malidhafi dhaifu hazifai kwa kutengenezea ngazi.


Vivi anakuwezesha kupendezesha nyumba yako. Simu 0755200023

Thursday, March 10, 2016

MITO YA ORANGE YA KWENYE MAKOCHI

Hey wapenzi, kununua muonekano huu njoo 0755 200023. Unaletewa hadi ulipo..

Tuesday, March 8, 2016

Milango ya mbao ngumu ndio bora zaidi kwa nyumba yako

Kwa uimara na viwango, milango ya mbao inaipa nyumba muonekano wa mvuto wa kipekee.
Mukhangu Noah ambaye ni fundi milango anasema kuwa kati ya milango inayotengenezwa kwa malighafi mbalimbali ni muhimu kuchagua milango ya mbao ya mkongo, mninga au mnazi ukilinganisha na

Monday, March 7, 2016

Faida 4 za wallpaper ambazo huwezi ukazidharau

Ubunifu ni sanaa, na namna ambavyo unapendezesha mahali unapoishi ndio mfano hai wa jambo hili. Wakati unapoamua kupendezesha ukuta wa nyumba yako unaweza kuchagua kati ya rangi na karatasi za ukutani zijulikanazo zaidi kama wallpaper. Vitu vingi kama rangi, mguso, michoro na maua unaviangalia wakati huo. Ila ukiamua kuweka wallpaper unapata vitu hivi vyote kwenye kifurushi kimoja.

Kubandika wallpaper ndio hata rahisi zaidi ukilinganisha na mchakato mzima wa kupaka rangi.
Hapa naorodhesha faidia 4 utakazopata kutokana  na kubandika wallpaper kwenye ukuta fulani wa nyumba yako. Faida hizi ni za msingi na si za kudharau:

·         Zinadumu muda mrefu - Zinafaa kwa matumizi yoyote na kwa mtu yeyote katika chumba chochote iwe ni bafuni, chumba cha kulala au cha chakula. Wallpaper inaweza kudumu hadi miaka 15 na hata ukuta ukipata alama ndogo za nyufa, kwenye wallpaper hazitokezi.

·         Rahisi kusafishika - Ni rahisi mno kusafisha wallpaper kwa kitambaa kilicholoa. Hii inakusadia kuondoa vumbi au uchafu mwingine kwa haraka mno bila kuacha alama yoyote ukutani. Na nzuri zaidi unaweza kuchagua aina ya wallpaper ambayo ni ngumu kiasi kwamba unaweza hata kusafisha kwa sabuni na brashi.

·         Ni rahisi kubandika na kubandua - Huenda nawe ni mmoja wa wanaohofia kuwa kubandika au kubandua hizi karatasi za ukutani kutasababusha uharibifu wa ukuta. Sii kweli, nyingi ni rahisi tu kubandua na kubandika tena kama umeamua kubadili muonekano kwa kubandua za zamani na kubandika mpya.

·         Gharama nafuu - Endapo utaamua kubandika wallpaper ni kwamba baada ya muda utagundua kwamba ingekuwa ni kupaka rangi ungetumia gharama kubwa zaidi. Hii ni kwasababu wallpaper zinadumu miaka mingi ukutani kinyume na rangi. Pia kama unataka dunia zote mbili yaani ya wallpaper na ya rangi basi kuta fulani za chumba unabandika karatasi wakati zile nyingine unapaka rangi.

Uamuzi wa kuingia kwenye ulimwengu wa wallpaper ni wako wewe mwenye nyumba!


Ninakuwezesha kupendezesha nyumba yako. Piga/whatsapp 0755 200023

Dondoo za namna ya kuchagua fimbo za pazia


Ni rahisi kutozingatia namna pazia na fimbo zake zinavyofanya chumba kionekane. Ila pale unatapoziondoa ndipo unagundua umuhimu wake. Zifuatazo ni dondoo chache za namna ya kuchagua fimbo kwa ajili ya pazia unazotaka kutundika.

Weka fimbo ambazo zinaendana na mapambo mengine ya chumba husika. Hapa ni muhimu kuangalia rangi ya fimbo. Usijeukanunua fimbo za rangi ya dhahabu kwa mfano, isioane na

VIATU HIVI VYA SHANGA VIPO

Usijali juu ya kwamba una mguu mpana au mnene. Iwe iwavyo utatengenezewa kiatu cha kukufaa. Viatu vyetu ni vya ngozi kamili na shanga original. Bei ni elfu 25. Kununua piga au whatsapp 0755200023


Saturday, March 5, 2016

PICHA NZURI ZA UKUTANI SET YA PISI 3

Picha za ukutani moja kubwa na mbili ndogo. Bei ya zote tatu ni sh laki moja. Kununua njoo 0755 200023

unaweza kuzitundika kwenye level moja kama hivi na umbali kati ya picha na picha usizidi inchi 2

Au unaweza kunyanyua kubwa ya kati juu na hizi ndogo zikakaa level moja fasheni hii.


CAR SHADE, MIAVULI YA BUSTANI NA TURUBALI ZA KUZUIA JUA

Usikubali rangi ya gari lako iharibiwe na jua. Tujulishe tukusimikie net ya car shade kama hii



Weka mwavuli bustanini ufaidi mahali pa kupumzikia kupunga upepo

Hii ni kwa ajili ya sehemu ambapo jua linaingia ndani na kuwa kadhia kwa kuwachoma waliomo.

Kwa mahitaji tuwasiliane 0755 200023

PICHA NZURI ZA UKUTANI ZINAPATIKANA

Hey friend, natumai jumamosi ni njema kwako. Wewe unayehitaji picha nzuri za ukutani sasa zinapatikana, zina sehemu ya kutundikia kwa nyuma (naamaanisha sio za mezani) na ukubwa wake ni upana wa cm 28 kwa urefu wa cm 35. Ziko chache. Simu 0755 2000 23
Inafaa kuwekwa kwenye corridor

Inafaa dining
Inafaa bedroom juu ya ubao wa kichwani

Maua sebuleni na kwenye corridor yanapendeza



Thursday, March 3, 2016

VMC:....MITO MIDOGO YA KWENYE MAKOCHI YA ORANGE SASA IPO


Rafiki, hivi unajua kubadilisha mito au foronya ndio njia nyepesi na gharama nafuu kuliko zote ya kupendezesha sebule yako? 

Mito hii ya orange inafanya kazi kubwa ya kuongeza rangi kwenye makochi, na ubora wa kitambaa chake ni wa uhakika. Kununua nijulishe. Bei ya mto pamoja na foronya yake ni elfu 25. Bei ya foronya pekee ni elfu 20. Karibuni..

PICHA: Mpangilio wa stoo ya vyakula

Mpangilio ni kiini cha usafi ndani ya nyumba. Mara utakupoweza kupangilia utakuwa umejikomboa jumla.

Wednesday, March 2, 2016

TRAY NZURI ZA MBAO ZINAPATIKANA



Tray nzuri za mbao sasa zinapatikana. Zina muonekano wa kuvutia wa asili na finishing yake maji yanateleza. Set moja ina tray 3. Zipo chache na endapo unahitaji karibu. Piga/whatsapp 0755200023

HOME DECOR HAPA NA PALE.....TABLE RUNNER, PAZIA, TAA ZA JIKONI

Nimependa hii meza ambapo table runner zimetandikwa kwa upana. Just kuwa mbunifu usitandike kwa urefu tu saa nyingine unabadili muonekano. Watu wanapenda mabadiliko!
Chumba ni pazia, vilevile tazama utundika wa zile sanaa za ndege ukutani. Pata idea za utundikaji wa picha pale sehemu kubwa ya chumba inapochukuliwa na pazia.
Wengi wanapojenga jiko wanazingatia zaidi makabati na kutotia maanani vitu vidogo kama taa. Hizi taa za kuning'inia kwenye housing lake (pendants) zinapendezesha jiko kwa mwanga wa kutosha.

Msisahau kushea na mimi picha za majumbani mwenu ili tujifunze pamoja. Ukishea ujuzi unajisikia vizuri!

Mambo matano unayotakiwa kufahamu kabla ya kuanza mradi wa kupendezesha nyumba yako


Hongera! Umeamua kuanza kuipa nyumba yako muonekano wa kuvutia. Kwa binadamu yeyote nyumba ni mali muhimu na ambayo iko karibu zaidi na moyo wake. Kila mwenye nyumba anatamani nyumba yake ionekane nadhifu na ya kuvutia  bila shaka kuliko sehemu yoyote ile nyingine kwenye ulimwengu huu. Hii ndio maana dhana ya kupendezesha nyumba iko kwa kila mtu.

Kama tujuavyo kupendezesha nyumba kunahitaji muda na fedha, hivyo unatakiwa kuwa makini sana na maamuzi yako. Mara tu unapoanza kufikiria jambo hilo, kuna mambo muhimu ya kuzingatia kabla ya

Tuesday, March 1, 2016

Namna ya kubadilisha muonekano wa nyumba na kuleta mvuto kwa gharama nafuu

Baada ya miaka kadhaa ya kuishi kwenye nyumba hiyo hiyo,  nyumba wengi wanatamani kubadilisha mionekano ya nyumba zao hizo. Na mara nyingi wazo linalowajia ni marekebisho ya jengo na kubadilisha fenicha. Hata hivyo hii inamaanisha gharama kubwa na kushirikisha wataalam wa kutekeleza jambo hilo.

Lakini je, kwanini mwenye nyumba asifikirie kufanya mabadiliko ya gharama nafuu kama vile badala ya kununua fenicha mpya akafanya maboresho kidogo ya zilizopo na zikaleta mvuto kabisa.

Makala zangu nia yake ni kukupa mawazo lukuki ambayo unaweka kutumia kuboresha maisha ya nyumbani kwako kwa gharama nafuu. Endapo mwenye nyumba utaamua kufanya utafiti kidogo na kufuata ushauri unaweza kufanikisha kazi yako kirahisi na kwa gharama nafuu sana. Kwani utakuwa umeshaelewa picha nzima ya unachotakiwa kufanya na kwa wewe kushirikiana na watendaji wachache utafanikisha lengo lako.

Matumizi tofauti ya rangi, karatasi za ukutani, vitambaa na malighafi nyingine zilizotengenezea fenicha zako vinaweza kubadilisha kabisa muonekano na kukupa wa kuvutia.
Zipo rangi za kung’aa kama polishi na zipo zisizong’aa za mati unazoweza kutumia kuboresha fenicha zako. Kwa mfano kupaka rangi upya kabati la luninga,  miguu ya kiti au meza kunabadilisha kabisa muonekano wake. Vile vile bila kusahau kubadilisha kitambaa kilichotengenezea viti au sofa endapo kuna umuhimu wa kufanya hivyo.

Dondoo nyingine ni kubadili vitu kidogodogo kama vile tai na fimbo za pazia. Ni ukweli kuwa vitu vya nymbani vinabadilika kila baada ya kipindi kifupi. Huenda tai zako za pazia za miaka mitano iliyopita ni tofauti kabisa na zilizopo kwenye mitindo sasa. Cha muhimu ni kuangalia hivi vitu vidogo visivyo vya gharama kubwa ambavyo ukivibadili vinapendezesha nyumba yako zaidi.

Eneo lingine ni la kwenye mito ya makochi. Kuwa na foronya mbalimbali na badilisha mara kwa mara. Vilevile kwa upande wa bakuli la taa, balbu siku zote ni hiyohiyo kinachobadilika ni jumba lake. Endapo utabadili jumba la taa kama vile taa ya jikoni au chumba cha chakula na kuweka ya kisasa zaidi bila shaka utakuwa umeboresha muoneakno kwa gharama nafuu kabisa.
Tukienda kwa upanda wan je ya nyumba huenda ukataka kuboresha kwa kupaka rangi upya na pia kuongeza taa za ulinzi. Unapopaka rangi zingatia kuboresha zaidi yale maeneo yaliyomeguka meguka. Kwa mfano nimeona watu wakitengenezea mikanda kuzunguka madirisha ambapo mwanzoni haikuwepo. Matokeo ya hii mikanda ni kufanya nyumba kuwa ya kisasa zaidi kwa nje na vilevile kuficha zile kona zilizokuwa zimemeguka.

Kwa upande wa bustani huenda mwanzoni miaka ya nyuma uliweka njia ambazo sasa huzihitaji tena kwa maana ya kwamba hazitumiki. Ni wakati wa kuziondoa na kufanya eneo lote liwe na ukoka. Pia kuna wakati vitofali vinakuwa vimemeguka aidha kwa sababu ya maji ya chumvi au ni kwamba tu vimekaa muda mrefu. Kutokana na hali yake unaweza kuvipaka rangi au laa kuviondoa na kuweka  sakafu ya malighafi nyingine bora zaidi iliyopo sokoni kwa kipindi hicho. Wakati huohuo usisahau kuboresha stendi na  vyungu vyako vya maua aidha kwa kuvipaka rangi (kazi ambayo unaweza kufanya mwenyewe) au kuotesha maua mazuri zaidi.

Hizi ni dondoo za maeneo kadhaa unayoweza kuangalia ili kuboresha muonekano wa nyumba yako uwe wa kisasa zaidi na mahali pazuri pa kuishi. Na kama wewe ni mpenzi wa vitu vizuri hii inaweza kuwa ni tabia yako kila baada ya miaka kadhaa.


Vivi anakuwezesha kupendezesha nyumba yako kwa gharama nafuu kabisa, atakushauri na aidha utatekeleza wewe mwenyewe au atakuunganisha na watendaji wa maeneo hayo. Kwa maelezo zaidi simu 0755200023