Pages

Monday, July 25, 2016

Faida za kuwa na jiko la nje

Zamani ilikuwa kawaida kwa familia kuwa na nyumba kubwa ya kulala na nyingine dogo pembeni ya jiko. Uwepo wa nyumba za kisasa zenye chumba cha jiko ndani yake unapelekea kupotea kwa dhana ya kuwa na jiko la nje.

Iwe unajenga nyumba mpya au unaifanyia marekebisho hiyo ya zamani, kwenye makala haya nitakuonyesha faida kadhaa za
kuwa na jiko la nje:

1. Linakufaa sana wakati wa sherehe nyumbani
Faida kuu ya kwanza ya kuwa na jiko la nje ni kwamba linakufaa sana wakati wa sherehe nyumbani. Chakula kinapokuwa kinaandaliwa huku ukiwa na wageni wako bustanini utashangaa ni kwa namna gani unavyoweza kumburudisha kila mmoja bila ya kuwa na sababu ya kuingia kwenye nyumba kubwa. Kumbuka hii ni nzuri kwani nyumba inabaki safi na kwenye mpangilio kama ilivyokuwa awali hivyo kuepuka kero ya kusafisha baada ya sherehe.
Pia wakati wa burudani watu wanapenda kuwa karibu na jiko, kuona ni nini kinachopikwa au kuchomwa. Ni sawa na hulka ile ile ya wengi kupendelea kukaa kwenye mabaa. Unachotakiwa kufanya tu ni kuwa na viti vya kutosha wageni wako, mwanga na mziki!

2. Linaongeza thamani ya nyumba
Unapokuwa na jiko la nje lililokamilika kwa kuwa na vifaa vyote vya msingi utagundua ni kwa namna gani hata msaidizi wako wa nyumbani anaweza kulitumia kuandaa chakula pale ambapo haupo nyumbani na pengine hutaki au humuamini kwa matumizi ya jiko la ndani.

3. Linarahisisha mapishi
Kuna wakati unahitaji mapishi ya aina mbalimbali labda ni chomachoma, kukaanga samaki na vyakula vingine vya baharini, ambapo mapishi haya yanazalisha harufu kali. Unapokuwa na jiko la nje unahamishia mapishi ya namna hiyo kule.
Pia jiko la nje linasaidia kuepusha uzalishaji wa joto ndani kama tujuavyo kupika kunazalisha joto. Fahamu kuwa jiko la nje kama lile la ndani linaweza kuwa na vifaa vyote muhimu jikoni.


4. Linaongeza ukubwa wa makazi
Unapokuwa na jiko la nje unajikuta kuwa kama familia mnatumia zaidi eneo la nje ya nyumba kwa matukio mbalimbali kama vile ya siku ya kuzaliwa, sikukuu au hata kufurahia mandhari ya nje tu badala ya kufanyia kila tukio ndani.

5. Linahamasisha mapishi ya vyakula bora
Sio tu kwamba vyakula vya mapishi ya kuchoma vina ladha nzuri, ni kwamba mapishi ya namna hii ni mazuri pia kwa afya bora kwani wakati wa kuchoma mafuta mengi yanaondoka kwenye nyama kwahivyo kile kinacholiwa kinakuwa kina kiasi kidogo sana cha mafuta. Kama una mkakati wa kupunguza unene bila shaka mapishi ya kuchoma ndio mazuri zaidi kwako.
Choma mwenyewe nyama nyumbani badala ya kuzifuata kwenye mabaa, siku zote chakula cha kuandaa mwenyewe kinaaminika kuliko cha sehemu za biashara.

Kwa ushauri piga 0755 200023

No comments:

Post a Comment