Pages

Thursday, September 8, 2016

Kabati la nguo la chuma ni suluhisho jepesi na la haraka


 
Kabati la nguo la chuma ni mkombozi kwako wewe unayeteseka kwa kukosa eneo la kuhifadhia nguo zako. Katika hatua fulani ya maisha wengi wetu tulishakumbana na hili tatizo, labda ni kwenye hosteli, chumba kidogo au kwenye nyumba ya kupanga ambapo huwezi kufanya marekebisho makubwa kwakuwa wewe sio mmiliki. Kuweka mpangilio ndani ya nyumba inawezekana kuwa rahisi kabisa na
siri ni kabati la nguo la chuma.

Nimehojiana na Muse Marwa wa kampuni ya Metals Tanzania ambao ni watengenezaji wa bidhaa nyingi za chuma kwa ajili ya majumbani na hapa anatujuza faida za kuwa na kabati la nguo la chuma. Anasema faida mojawapo ni kwamba yanatengenezwa kwa ukubwa na miundo mbalimabali, kwahivyo ni rahisi kupata lililo sahihi kwa chumba unachotaka kuliweka.

Kwa asili ni makabati imara sana na ni sahihi kwa kubeba vitu vizito. Ni rahisi pia kusafisha na ukishapaka rangi ya mwanzo ni mara chache sana kuwa utalipaka tena rangi kwa maisha yote.

Japo tumesema kuwa kabati la nguo la chuma ni imara kuliko la malighafi nyingine yoyote, ni vyema pia kufahamu kuwa ni rahisi kubebeka kuhamisha kutoka chumba kimoja hadi kingine ukilinganisha na la mbao kwa mfano.

Kutokana na kwamba miundo ya makabati mengi ya nguo ya chuma ni myepesi ni rahisi kupanga nguo, na yana maeneo kadhaa ya kuwekea vitu kama  viatu, pochi, mikanda na vitu vingine vyovyote unavyotaka kuhifadhi humo kwa sababu liko wazi eneo kubwa kwahivyo vitu vinaonekana vizuri. Na vilevile kutokana na uwazi wake kuna faida nyingine kuwa panya na wadudu wengine kama mende, siafu au sisimizi hawawezi kujificha na kuishi kwenye kabati.

Watu wengi wenye bajeti ndogo wanapendelea makabati ya nguo ya chuma kwasababu ni gharama nafuu ukilinganisha na ya malighafi nyingine kama mbao. Kwa mfano kabati la nguo la mbao ngumu linalogharimu kiasi cha shilingi laki 8 likiwa la chuma la ukubwa huohuo linagharimu nusu ya bei hiyo. Lakini ingawa ni bei rahisi yanadumu daima dumu.

Faida nyingine ya kabati la nguo la chuma ni kwamba linachukua nafasi ndogo ya chumba na vilevile unaweza kulipachika kwenye eneo lililotengwa tayari kwa ajili ya kabati.

Mbali na kuwa kabati la nguo ya chuma ni rafiki kwa mazingira kwa kuepuka kukata miti hovyo bali pia mengi ya makabati haya yanatengenezwa na wajasiriamali wa hapahapa nchini kwa hivyo ni muhimu kuunga mkono maendeleon haya ya viwanda vidogo ili kukuza uchumi wetu.


Faida hizi zinafanya makabati ya nguo ya chuma kuwa chaguoo zuri katika kuhifadhi nguo zako.

Mawasiliano ya Metals Tanzania kwako unayehitaji fenicha za chuma ni Bi Musse Marwa simu 0716 215 531 email: mussemarwa@yahoo.com

No comments:

Post a Comment