Pages

Sunday, January 31, 2016

KUTOKA KWANGU:...Siri ya kupamba nyumba kwa gharama nafuu


Ukitaka kufanikiwa katika jambo lolote ni muhimu kuwa na mipango iliyoandaliwa. Vilevile katika mapambo ya nyumba mipango ni jambo muhimu.

Kama toka awali

Saturday, January 30, 2016

PICHA:.....NI NINI KIPO KWENYE ENEO LA MIGUUNI MWA KITANDA CHAKO?


Unapokuwa na fenicha kwenye eneo la miguuni mwa kitanda chako kunakupa faida kuu mbili. Moja ni eneo la kukaa hasa unapokuwa unajiandaa kutoka. Yaweza kuwa ndio unavaa au unapata kifungua kinywa cha chumbani.

Pili ni eneo la kuhifadhia bed runner na mito yako unayotumia kupamba kitanda lakini usiku huitumii. Badala ya kuitupa sakafuni basi iweke hapo.

Je wewe eneo la miguuni mwa kitanda chako umeweka nini? Nitumie picha 0755 200023

PICHA: Style ya mlango wa mbele, upi umekubamba?


Kati ya hii milango miwili ni wa style gani ungechangua kuwa mlango wako wa mbele, je ni pembe nne au yai?

Usisahau kunitumia picha ya mlango wako wa mbele. Ukishea ujuzi unajisikia vizuri!

Friday, January 29, 2016

HOME DECOR HAPA NA PALE:...DARI LA RANGI, SHELFU ZA VYOMBO, GROUT

Friends, ni post nyingine tena ya kuangalia kunani hapa na pale kwenye mapambo ya nyumba, enjoy!
Hizi ni dari za rangi, kuna wenye nyumba wanaopenda rangi kiasi kwamba wanaweka hadi kwenye dari. Kwa picha hizi unaweza pata idea ya namna dari za rangi zinavyokuwa. Niliweka post hapa hadi wapo wanaoweka wallpaper darini. Kumbuka ni nyumba yako ladha yako.
Wakati mwingine kama kuna uhakika wa usalama hasa familia zenye watu adults shelfu za wazi za kuhifadhia vyombo zinafaa kuliko makabati. Kwanini? Kwasababu kwanza, uzuri wa mpangilio unaonekana halafu pia ni rahisi kutoa na kuweka vyombo. Nitakapofikia umri fulani nadhani nitaenda na open shelf jikoni..ha hahaaaa. Tuombe uzima

Grout ikichafuka au kumeguka unaweza kujikuta unachukia floor yako. Ila habari njema ni kwamba kwa tiles hizo hizo unaweza kufanya marekebisho kwa kuweka grout mpya. Grout mpya ni wazo zuri zaidi hasa bafuni kwenye zile tile za chini ambapo grout inabadilika rangi au kuchakaa kwa ajili ya maji na uchafu. Usilichukia bafu, unachotakiwa ni kujaza grout upya.

Niambie hapa na pale kwenye mapambo yako ya ndani kunani?..Tuwasiliane

Thursday, January 28, 2016

PICHA: Siri ya kuwa organized ni kuwa ni kuwa na vitendea kazi



Friends, naona wengi wanahangaika sana kujua jinsi ya kupanga chumba, jinsi ya kupanga kabati la nguo, jinsi ya kupanga vyombo jikoni na jinsi nyingi za kuweza kuwa na mpangilio. Siri kuu ni kuwa na vitu vya kukuwezesha kuwa na huo mpangingilo. Kwa maana ya kwamba labda una nguo zimejazana kwenye kiti/kochi, bila kuwa na kabati la nguo au kitu simple tu cha kukuwezesha kutundikia nguo zako na kingine cha kuweka zile za kukunja kamwe huwezi kuwa organized. Kwa hiyo bottom line ni kwamba mpangilio unaendana na uwepo wa vitendea kazi vyake ambavyo naweza kuviita ni vihifadhio.

Nawe nishirikishe vihifadhio vyako hapo nyumbani kwako. Ukishea ujuzi unajisikia vizuri!


Wednesday, January 27, 2016

KUTOKA KWANGU:....Rangi sahihi katika chumba cha wakuu wa familia (MASTER BEDROOM)

Rangi sahihi zitakifanya chumba cha wakuu wa familia kama mahali patakatifu. Kuchagua rangi kwa ajili ya kupaka chumba cha wazazi (master bedroom) ni moja kati ya hatua kubwa unazochukua wewe mwenyenyumba  za kutengeneza  mahali binafsi. Chaguo lako linatakiwa liendane na

KUTOKA KWANGU:....Dondoo 7 za kuongeza mwanga kwenye chumba chochote


Wengi wetu tuna vyumba ndani ya nyumba zetu ambavyo havipati mwanga wa kutosha kiasi ambacho tungependa iwe. Pazia nzito, zulia au sakafu ya rangi za giza na rangi ya ukutani isiyo sahihi vinaweza kuwa ndivyo vinachangia chumba kisiwe na

HOME DECOR HAPA NA PALE:...KIZULIA CHA JIKONI, TABLE RUNNER, BEDROOM YA WATOTO WA KIUME

Friends, hebu tutazame picha za vyumba hizi tujifunze kitu. Tusijali kama ni mazingira ya uzunguni kwani hata sisi kibongobongo inawezekana...binadamu ni mmoja mazingira ndio tofauti.
Hapa nataka tuangalie hiki kizulia cha jikoni. Miguu inaburudika kukanyaga zulia hasa pale inaposimama muda mrefu. Kwa jikoni unaweza kutupia kizulia maeneo kama kwenye sink na cooker. Kama jikoni kwako tayari umeshatupia tafadhali nitumie picha..
Hapa katika hii meza ya chakula nataka uone namna nyingine ya kutumia table runner. Wengi tumezoea ile runner ya kupita kati tu, kumbe unaweza kutupia runner mbili, tatu au nne kuendana na ukubwa wa meza yako zikawa na kazi 2; mapambo na mats.
Hiki chumba cha watoto wa kiume ona jinsi vitanda simple kabisa vya chuma vilivyokaa vizuri. Wakati mwingine nyumba kupendeza si pesa ndefu bali ni ubunifu na kuwa na fikra pana hasa kujitahidi kujua option nyingi kabla hujaamua jambo. Na hapa ndipo unakuja umuhimu wa ushauri wa mtaalam. Kitanda kimoja kama hiki kinaweza hata kisifike laki na nusu.

Pata ushauri wa busara kabisa wa mapambo ya nyumba na bustani yako toka kwangu..Let's meet 0755 200023

Tuesday, January 26, 2016

PICHA: KABLA na BAADA ya urembo wa kona za nje za nyumba

Kabla kona hazijarembwa zilikuwa hivi. Ukuta wote ulikuwa level sawa.
Baada ya kona kurembwa zikawa hivi.
Rangi ya kona na ya ukutani zote ni conmix lakini katika shades tofauti. Muonekano sawa wa bati, kona na skirting. Mwenye kufanya kazi hii ni Ras Jack simu 0656 599 111.

Kila panapowezekana kurembwa panarembwa mdau wangu. Ukihitaji ushauri kwa lolote la kuhusu namna ya kupamba nyumba au bustani yako usisite kunijulisha.
Let's meet 0755 200023

Do you love me?

Friends, valentine ndio inakaribia na kwenye collection yangu kuna vitu vizuri na unique ambavyo huwezi kukosa kimojawapo kwa yule umpendaye.. enjoy...





Kama unavyoona kuna sandals nyingi na za staili mbalimbali za kike na za kiume na ni handmade kwa ustadi mkubwa sana na ni full ngozi. Pia kuna hiyo mishumaa yenye perfume na kuna table runner za uhakika. Karibu ununue kutoka kwangu. 
Let's meet 0755 200023

MBWA ANAWEZA KUWA NI WA PAMBO, HOBBY, BIASHARA AU ULINZI.....Amini usiamini anauzwa hadi dola 800!

Neema akiwa na mbwa wake scooby kwenye gari. Anasema scooby ni mpole anasafiri naye hahangaiki, mkewe ni mjamzito kwahivyo anategemea kupata wajukuu soon..lol

Monday, January 25, 2016

KUTOKA KWA MDAU:.....Urembo wa Skirting ya Nje ya Nyumba



Kama nilivyosema kwenye post za nyuma kuwa yale mambo ya kuotesha maua kugusana na ukuta wa nyumba yanaelekea kuishia, vilevile rangi kwenye skirting nayo inaishilia. Sasa hakuna cha skirting ya rangi nyeusi ya lami mara ooh rangi ya ugoro, chocolate hapana. Tunakoelekea ni decorations za mawe kama hivi kwenye skirting. 
 Fundi wa hii kazi anaitwa Said na namba yake ya simu ni 0762 341 233

Kama na wewe ni fundi na unafanya kazi za viwango nitumie picha za kazi zako, hujui ni nani anaweza kuziona na kukupa kazi zaidi. Pia ukishea ujuzi unajisikia vizuri.

Sunday, January 24, 2016

PICHA: Bodaboda wa mkoa wa Dodoma wamsalimia Lowassa NYUMBANI kwake baada ya kumuona akitoka kanisani leo.


Huwa nafurahia matukio kama haya kwa ajili yanatupa fursa ya kuona nyumbani kwa viongozi na watu maarufu.


KUTOKA KWANGU.....Unapohitaji fundi mzuri wa TILES, zingatia dondoo hizi

Kosa dogo tu katika uwekaji wa marumaru sakafuni au ukutani kwa jikoni na bafuni linaleta ukakasi machoni. Marumaru moja tu inapokuwa imewekwa vibaya ,  inaweza kuharibu mtiririko mzima na kufanya muonekano wa kupinda. Mbaya zaidi kufanya marekebisho baadaye, inaweza kuwa

Saturday, January 23, 2016

PICHA: Rais mstaafu JK ahani Msiba NYUMBANI kwa marehemu Mkurugenzi wa TAA



Raisi mstaafu JK akihani msiba NYUMBANI  kwa aliyekuwa mkurugenzi wa TAA (Tanzania Airports Authority) Mhandisi Suleiman S Suleiman aliyefariki dunia January 18 mwaka huu majira ya asubuhi wakati akifanya mazoezi ya kuogelea bahari ya hindi eneo la magogoni. Alizikwa jioni ya siku hiyohiyo. Mungu ampumzishe pema.

CHANZO: kajunason.com

PICHA:...JINSI UNAVYOWEZA KUTUMIA RANGI YA LAVENDER CHUMBANI

Lavender ni rangi fulani hivi jamii ya zambarau. Angalia jinsi unavyoweza kuitumia shade hii kwenye vyumba mbalimbali nyumbani kwako.
Ila kuwa makini usijeenda na ile zambarau ya misiba! 
Dining table vitambaa vya viti ni vya rangi ya lavender. Inapendeza eeh.. 
Love seat ya rangi ya lavender
Kitambaa cha sofa za rangi ya lavender. Wewe unayetengeneza sofa au unaye repair unaangalia nini unapochagua kitambaa?

Nitumie picha za jinsi ulivyotumia rangi hii nyumbani kwako. Hata kama ni kwenye flower vase tu. Ukishea ujuzi unajisikia vizuri!

Friday, January 22, 2016

PICHA: HIVI NDIVYO BONGO CELEB CHIBU DANGOTE ANAVYOSPEND JIONI YAKE

Mwanamziki mbongo fleva Diamond Platnumz ametupia picha hii kwenye ukurasa wake wa instagram akiwa anaogelea kwenye swimming pool la nyumbani kwake na kuandika..."Raha ya ustar uwe na yako nyumba sio shombo kuvunda!"

Msomaji kama na wewe una swimming pool nyumbani kwako au picha ukiwa kwenye swimming pool hebu nitumie tuone unavyospend mule...lol

VMC HAPA NA PALE:.......SANDALS, TABLE RUNNER / UTEPE WA MEZANI, PERFUMED CANDLES

Hii table runner ina urefu wa mita 1.9 (karibia mita 2) ziko ya rangi 2, hii ya kijani cha apple na ya gray. Table runner inafaa kupambia meza na pia kuweka mabakuli kama hivi wakati wa msosi ili meza isikwaruzike.
Table runner hii ya kiafrika zaidi kwa ukubwa wa coffee table na dining nazo zinapatikana.
Sandals kwa styles za kila aina bado zipo.
Mishumaa ndio inanunulika kwa kasi wahi fasta kabla haijaisha

Njoo ununue.

Umenunua bidhaa gani mpya mwaka huu?...Nishirikishe.

Thursday, January 21, 2016

KAMA ULIKUWA UNAJIULIZA ZAWADI YA VALENTINE BASI MISHUMAA INAYONUKIA NI HALALI YAKE

Hii mishumaa inanukia wakati wote iwe imewashwa au imezimwa. Scents (harufu) zilizopo ni vanilla, rose na lavender. Kama unahitaji tuwasiliane..

PICHA: NAMNA YA KUHIFADHI MIIKO NA VIJIKO VIKUBWA VYA KUPIKIA

Kuna faida kadhaa za kuwa na jagi au kikombe kikubwa jikoni kwa ajili ya kuhifadhia miiko na vijiko vya kupikia
Vijiko na miiko vinapokuwa vimehifadhiwa mahali pamoja vinadumisha usafi wa kaunta za jiko. Hiki kikombe/jagi ni lolote tu just kuwa mbunifu. Ukipata maalum kwa ajili hiyo ni poa vilevile. Huwa vinaandikwa utensil jar. 
.
 Vijiko na miiko vinapokuwa vimehifadhiwa mahali pamoja vinaokoa muda wa kutafuta kimoja kimoja wakati wa kupika. 
Vijiko na miiko vinapokuwa vimehifadhiwa mahali pamoja vinadumisha mpangilio wa jiko.

Nawe msomaji asante kwa kutembelea blog yangu na pia nishirikishe jinsi unavyohifadhi miiko na vijiko unavyopikia. Ukishea ujuzi unajisikia vizuri!