Tuesday, May 4, 2021

MSHAURI AKIKUPA MAJIBU HAYA NI KWAMBA HANA MSAADA UNAOHITAJI

 FOLLOW INSTAGRAM @vivinavisavyake



Wengi wetu tumeshapitia changamoto za kimahusiano ambapo kumueleza mtu tunayemuamini huwa inatupa ahueni au msaada ambao utatuvusha.

Kama huyo unayemuamini na kumwendea kumueleza anakupa majibu haya ina maanisha kwamba aidha jambo lako ni kubwa sana kwake kuweza kulichakata na kukushauri cha kufanya ama hataki kujishuhulisha nalo.

Hivyo anaweza kukupa baadhi au mojawapo ya sentensi hizi. 
1. Kila kitu kinatokea kwasababu.
2. Liombee tu
3. Muda utasema
4. Achana nalo
5. Usiliongelee tena
6. Utakua sawa ukijaribu kulisahau
7. Acha kulifikiria utajisikia vizuri
8. Kuwa imara tu
9. Maisha ndivyo yalivyo
10. Ambacho hakijakuua kinakufanya imara
11. Ingeweza kuwa mbaya zaidi.

Ukishaona majibu hayo hapo juu, aga tu kwa uzuri na usirejee kwake kwani hutapata msaada unaotaka.
Muhimu ni kwakuwa umeshajua basi usikate tamaa bali tafuta msaada kwingine.

Kama una changamoto ya mahusiano njoo tuzungumze simu 0755200023

 


No comments:

Post a Comment