Monday, September 18, 2023
NINA MAFUTA YA KUONDOA MAKUNYANZI
Rejuvenating cream inaondoa mikunjo kwenye ngozi yako ya uso na mikono ili kukurejesha katika muonekano wa ujana.
Thursday, September 14, 2023
LOTION YA KUONDOA MAKOVU, WEUSI NA ALAMA NYEUSI
BODY LUV
imekamuliwa kutoka kwenye mafuta ya mimea, Hii bidhaa ni nzuri ,hasa hasa kwenye zile sehemu zinazoshika weusi Kwa haraka.. mpajani, sugu zote, kwapani, na wale wenye makovu sehemu yoyote.
๐ MATUMIZI unaipaka kabla ya kuoga sehemu zenye weusi unakaa nayo dakika 5 baada ya hapo unaenda kuoga na kuacha sehemu ya weusi ikiwa Laini ..
๐Pia Ina harufu nzuri na hainati inasambaa yenyewe Tena Kwa urahisi inapokutana na maji
๐Inazuia ukavu wa kukatika Kwa ngozi haswa magaga na kuacha ngozi yako ikiwa laini
Call/watsp
0628645231 au 0755200023
@_neolife_tip
Njoo Kuna Fursa ya Vipodozi na Bidhaa za Afya na Usafi
Nina Fursa. ๐
Njoo Whatsapp 0755200023
TUNAHITAJI MAWAKALA
Na PIA TUNAUZA BIDHAA KWA BEI YA KAMPUNI
MAWAKALA MTAJI NI 370,000/=
WANUNUZI WATAPEWA BEI ELEKEZI WATSP
CALL/WATSP
0628645231
@_neolife_tip
Thursday, July 27, 2023
MAMA BEYONCE AOMBA TALAKA NDOA YA PILI
Mama yake #Beyonce, Tina KnowlesLawson (69) ameomba talaka kuvunja ndoa yake ya mara ya pili ili aachane na mumewe Richard Lawson (76).
Kwa mujibu wa nyaraka za kisheria zilizopatikana na mtandao wa TMZ, Tina ameanza mchakato wa kuomba talaka jumatano iliyopita.
Kwenye nyaraka hizo inaripotiwa Tina ameainisha sababu ya kutaka kuvunja ndoa ni tofauti zisizorekebisha pia ameomba baada ya talaka mahakama imrejeshee jina lake la mwanzo Celestine Knowles na pia kusiwe na matunzo ya mwenza (spousal support).
Ndoa ya Tina na Richard ina miaka 8, walioana 2015 ndoa iliyofanyika kwenye boti huko California na waalikwa wote walivalia white si baadhi yenu mnakumbuka mapichapicha eeh.
Mara ya kwanza Tina aliolewa na baba yake Beyonce, Mathew Knowles toka 1980 hadi 2011 na wakafanikiwa kuzaa mabinti wawili Beyonce na Solange.
Ndoa ya baba na mama Beyonce ilivunjika baada ya kugundulika Mathew wakati huo akiwa meneja wa kundi la kina Beyonce la Destiny's Child kazaa nje ya ndoa na muigizaji Alexandra White mtoto wa kiume anayeitwa Nixon Knowles aliyezaliwa 2010.
Awali Mathew alikataa Nixon sio mwanae lakini baadaye vipimo vya DNA ikathibitika ni mwanae.
Ndipo ndoa ya mama na baba Beyonce ikavunjika kwa mama Beyonce kuomba talaka na baada ya hapo kila mmoja akafunga ndoa mpya ambapo baba Beyonce alimuoa modo Gena Charmaine Avery toka 2013 hadi leo wako pamoja.
Wiki chache zilizopita Alexandra amehojiwa na jarida la Uingereza la the sun akasema mwanae Nixon hana ukaribu na dada zake (kina Beyonce na Solange) wala baba yake (Mathew Knowles).
Yani familia ya Knowles haitaki kujihusisha na Nixon.
Tuesday, July 25, 2023
HASIRA ZIMECHANGIA KUVUNJA NDOA YA DULLA MAKABILA
Kuhusu waliokua wanandoa #DullaMakabila na #Zaiylissa kuachana; Zaiylissa amefunguka " Nimemuacha kwasababu nimechoka, hajatulia na ana hasira sana".
Zaiylissa amesema ni kweli amepewa talaka 3 kwa mpigo ambazo Dulla aliziweka kwenye bahasha na zikawasilishwa nyumbani kwa Zaiy Chamanzi.
Akielezea maisha ya ndoa kwa miezi miwili na siku 10 alizoishi na Dulla; Zaiy amesema Dulla alikua na matukia ya rejarejaja yasiyo na kikomo ikiwemo kumfumania na meseji za warembo wa mjini na akimhoji anaambulia kipigo.
" Sio rahisi kuishi na Dulla kwa ajili ana kashkashi nyingi na hata wakati naolewa baadhi ya ndugu zake waliniita pembeni na kunisihi Dulla hajatulia niwe naye makini", ameeleza Zaiylissa, akaendelea kusema kuwa amejitahidi sana lakini uvumilivu umemshinda ameamua kuchapa lapa na kusepa.
Zaiylissa akaendelea kufunguka kuwa tokea awe kwenye mahusiano na Makabila hakuwahi kuchepuka hali ambayo hadi mume alimuuliza mbona huchiti maana kila akipekua simu hakutani na sintohamu yoyote.
Zaiylissa akamalizia maelezo yake kwa kusema kingine kilichofanya ndoa na Makabila imshinde ni kwamba Dulla ana hasira sana ambazo mara zote ziliishia mwilini mwa Zaiy kwa kipigo.
Monday, July 24, 2023
NDOA YA DULLA MAKABILA IMEVUNJIKA
Nyota wa muziki wa Singeli Tanzania mwanamuziki Dulla Makabila amekiri kuwa ndoa yake na muigizaji wa tamthilia ya juakali Zaiylissa imevunjika.
Tetesi za kuvunjika ndoa hiyo zilianza mwanzoni mwa wiki iliyopita baada ya mkewe kuondoa picha zao zote za pamoja na kumu unfollow mumewe kwenye account ya instagram.
Leo julai 24, 2023 Dulla akihojiwa na kipindi cha radio kwa njia ya simu amekiri ni kweli ndoa hiyo imevunjika.
Aidha kuna picha na video zinazomuonyesha Zaiylissa akiwa na vidonda vibichi vinavyochuruzika damu ikiaminiwa vimetokana na kipigo toka kwa ex wake.
Dulla na Zaiylissa walifunga ndoa may 12. 2023.
Ndoa ambayo imedumu kwa miezi miwili.
Miaka ya nyuma wote walishafunga ndoa na wapenzi wengine ambazo nazo zilivunjika.
Kwa Matangazo wasiliana na 0755200023.
MCHEKESHAJI JAYMONDY ANADAIWA KUMTELEKEZA MWANAE BAADA YA KUPATA GIRLFRIEND MZUNGU
Mchekeshaji #Jaymondy anadaiwa kutelekeza mtoto kisa kapata girlfriend mzungu.
Akieleza kwa uchungu mzazi mwenza wa mchekeshaji huyo amesema kipindi cha nyuma Jaymondy alikua anatoa matunzo ya mtoto na hata wao kama wazazi walikua na mawasiliano mazuri; lakini baada ya mzazi mwenzie huyo kupata mzungu mambo yamebadilika kabisa.
Baby mama huyo amesema mpasuko kati ya mzazi mwenzie na wao (mama na mtoto) ulianza kutokea baada ya Jaymondy kupata mzungu.
"Mapenzi yameisha kabisa kwa mtoto na hata hakumbuki ni lini kamjulia hali mtoto".
"Mtoto amefukuzwa shule ada na baba yake anaonekana mitandaoni akila raha Ulaya na hata alivyoondoka hakumuga mtoto", amesema baby mama wa Jaymondy.
Baby mama akaendelea kueleza kwa uchungu;
"Mzungu amefunga kila sekta hakuna mawasiliano kabisa."
Kwa sasa Jaymondy anaishi Scandinavia na mwanamke wake mzungu.
Saturday, July 22, 2023
TRACY NABOKERA NDIYE MSHINDI WA MISS TANZANIA 2023
Kampuni ya The Look chini ya Miss Tanzania Organization jana julai 21, 2023 imemtangaza mlimbwende Tracy Nabokera kuwa ndiye mshindi wa miss Tanzania 2023.
Kutangaza Biashara yako hapa wasiliana na 0755200023
SALUNI YENYE MANDHARI NZURI YA KUCHA NA NYWELE MWENGE DAR ES SALAAM
Je unatafuta salon yenye mandhari nzuri, safi na tulivu kwa ajili ya kusuka nywele zako na kutengeneza kucha?
OFFER RANGI YA GEL *5,000 NA KUBANDIKA KUCHA NA GEL *10,000* ☎️0787595342. ๐
๐ฝ๐
๐ฝ๐
๐ฝ *At Glow & Beauty*
@mwenge_salons #glow & beauty
Ghorofa ya kwanza - Jengo la Jamirex MWENGE SOKONI - Juu ya AZANIA BENKI.
*Parking zipo za kutosha*
๐ ๐
@mwenge_salons …. AT-GLOW & BEAUTY ๐
๐ฝ๐
๐ฝ๐
๐ฝ
Karibuni sana ๐๐๐ ๐
๐ฝ๐
๐ฝ๐
๐ฝ
#gelnails
#nails
#tanzania #daressalaam
#mwenge
#naturalhairstyles #makeup #kucha #kusuka #nywelezamkono #cornrows #twist. #crochet #rasta #jamirexhotelmwenge
@mwenge_salons
@vivimachangeblog
Thursday, July 20, 2023
WANANDOA PRINCE HARRY NA MEGHAN MARKLE WANADAIWA KUTENGA MUDA KUISHI KILA MMOJA KIVYAKE
Ripoti mpya kutoka mtandao wa #RadarOnline inadai kuwa wanandoa #PrinceHarry na mkewe #MeghanMarkle wamejipa likizo kila mmoja anaishi kivyake kwa sasa wakijitafakari ni hatua ipi ifuate katika ndoa yao baada ya misukosuko iliyotokana na madili yao kufeli.
Msongo wa mawazo kati yao unaripotiwa kuanza baada ya kukosa dili la $ milioni 20 spotify na podcast yao Archetypes kushindwa kupata msimu wa pili, chanzo kimesema.
Vyanzo kutoka familia ya kifalme vinaamini Harry anajaribu 'kujitafuta' baada ya mabadiliko mengi toka aondoke kwenye kasri.
"Wanajitahidi kujitafakari ni nini kimewagonga', chanzo kimefunguka.
" Harry hafiti kwenye mishe za ulimwengu wa Meghan."
Aidha vyanzo hivyo vimeuambia mtandao wa Radar kuwa Harry ana tripu ya kwenda Afrika kufilimu dokumentari yake ya Netflix kwahivyo vinaamini safari hiyo itamuonyesha picha ya hatua inayofuata kwenye ndoa yake.
Safari hiyo ya Harry pekee inatarajiwa inaweza kuwa ndio kitu Harry anahitaji kwa ajili analichukulia bara hilo kama "nyumbani kwake kwa pili na mahali ambapo anajisikia zaidi kuwa yeye", chanzo kimesema.
" Kutawanyika kila mmoja bara tofauti inatarajiwa kuwasaidia kuona ni namna gani wasonge mbele."
Wakati huohuo vyanzo vimesema Meghan tayari ana wakala bomba kwa kum brandi, "anataka ajirandi yeye kama yeye atengeneza mamilioni", mtaalam wa maswala ya kifalme Daniela Elser amesema. "Ni kwa mara ya kwanza kila mmoja anajijenga kitaaluma kwa njia yake."
" Meghan na Harry wapo kwenye presha kubwa kifedha ili kuishi maisha ya kifahari ya California ikiwa ni pamoja na jumba lao la dola milioni 14 pamoja na ulinzi wa hali ya juu", chanzo kimesema.
Ndoa ya miaka mitano ya Prince Harry na Meghan Markle imepitia kashkashi nyingi zikiwemo baadhi ya media kubwa za Uingereza kuwakeka kwenye picha hasi, kuhamia California na kuachana na majukumu ya kifalme na kufunguka kwa kina hadharani mambo hasi waliyopitia kama wanandoa kwenye familia ya kifalme.
Nifollow instagram @vivimachangeblog
Kutangaza Biashara yako hapa wasiliana 0755200023
Tuesday, July 11, 2023
WALIO KISS MOI
Juzi jumapili julai 9, 2023 mchana video ilisambaa mitandaoni ya mgonjwa aliyekua amelazwa wodini katika hospitali ya Muhimbili akila denda na mwanamke.
Menejimenti ya Tiba ya Mifupa ya hospitali hiyo MOI imetoa ufafanuzi kuhusu uvunjifu wa maadili ya Kitanzania uliofanywa na mgonjwa huyo jina limehifadhiwa aliyekua amelazwa wodi namba 3A.
Mgonjwa amekiri kufanya kitendo hicho na mwanamke aliyedai ni mpenzi wake.
Kama ilivyodhaniwa na wengi wa waliotazama video hiyo ya kwamba mwanamke huyo ni muuguzi; MOI imebaini sio muuguzi wala mfanyakazi wa MOI na kwamba video ilirekodiwa na mgonjwa wa pembeni na tendo la denda kuendelea lilikatishwa na muuguzi wa zamu.
MOI inalaani na kukemea kitendo cha kurekodi video wodini na kuisambaza mitandaoni pia kitendo mgonjwa aliyekula denda kuvunja maadili ya Mtanzania kwani ni kinyume na miongozo ya wizara ya afya.
Aidha mgonjwa huyo pia
amewaomba msamaha Watanzania.
NiFollow instagram @vivimachangeblog
Kwa MATANGAZO ya Biashara nicheki 0755200023
DIVA AMETANGAZA KUACHANA NA MUMEWE
Mwanahabari mtangazaji wa media ya Wasafi Diva Malinzi aka Diva the bawse ametangaza kuachana na mumewe Sheikh Abdulrazak Salum.
Diva amesema Abdulrazak ambaye ni mtaalam wa mahusiano kupitia visomo vya dini ni mpigaji, muongo na mnyanyasaji na amewaonea huruma wateja wake (wa Abdul).
Diva anasema Abdul amemtesa sana kwa kipindi cha ndoa yao ya mwaka na nusu.
Diva aliwahi kusema Abdul ana watoto watano aliozaa na wanawake wengine mbalimbali na alijitolea kwa moyo mweupe kuwa mama yao wa nyongeza.
Nifollow instagram @ViviMachangeBlog
Kwa Matangazo ya Biashara nicheki 0755200023
Monday, July 10, 2023
BARNABA NA RAYA WAMEFUNGA NDOA
Mwanamuziki wa bongo fleva Barnaba na mpenzi wake wa muda mrefu Raya wamefunga ndoa.
Barnaba ambaye alibadili dini kufuata ya Raya sasa anaitwa Mohamed.
Kamati imezawadia shilingi milioni 2.
Raya mjasiriamali wa saluni ya kike ni mtoto wa muigizaji machachari Mama Kimbo.
Mama Kimbo akitoa nasaha zake amesema amefurahi sasa kuwa mkwe halali.
Kwa hadharani hii ni ndoa ya mara ya pili kwa Barnaba ambapo awali alimuoa mrembo Zuu Namela ndoa ambayo baadaye ilivunjika.
Barnaba na Zuu wamejaliwa mtoto mmoja anayeitwa Steve.
Barnaba na ex wake Zuuh wana mahusiano mazuri na wanashirikiana malezi ya Steve ambapo Raya naye mara nyingi anashea mitandaoni akiwa na mtoto wake wa faida Steve.
Nifollow instagram @ViviMachangeBlog
Sunday, July 9, 2023
PADRE AMEFARIKI ASUBUHI BAADA YA KULALA USIKU MZIMA NA KIPENZI CHAKE HOTELINI
Padre wa Kanisa Katoliki parokia ya St Peters Ruai nchini Kenya amefariki baada ya kulala na mpenzi wake usiku mzima hotelini huko Murang'a.
Padre huyo ambaye ametambulika kama Joseph Kariuki Wanjiku (43) amefariki jana asubuhi julai 8 baada ya kukimbizwa hospitali na mpenzi wake akishirikiana na baadhi ya wafanyakazi wa hoteli waliyokuwemo.
Ripoti ya polisi inasema wapendanao Joseph na kipenzi chake (32) waliingia hoteli ya Monalisa Delview Gatanga ijumaa jioni.
Padre akaanza kujisikia vibaya jumamosi asubuhi.
Mpenzi wa Joseph mwanadada ambaye jina limehifadhiwa naye anafanya kazi katika parokia aliyokua anahudumu padre Joseph.
Follow @vivimachangeblog
MATANGAZO 0755200023
Saturday, July 8, 2023
CCM Imemfukuza Uanachama Balozi Ali Karume
Taarifa ya kumuondoa kwenye chama imetolewa na katibu mwenezi wa mkoa huo Ali Timamu Haji kutokana na kikao kilichofanyika saa saba usiku wa kuamkia leo julai 8, 2023 chini ya Katibu wa CCM wa mkoa Amina Mnacho.
Hatua hiyo inakuja baada ya CCM kumpa onyo kutokana na kauli zake akidaiwa kukidhalilisha na kuwatukana viongozi wakuu hadharani.
Nifollow so @ViviMachangeBlog
Tangaza Biashara yako hapa wasiliana na 0755200023
Wednesday, July 5, 2023
MWANAFUNZI WA UHASIBU MTWARA AMEJIUA KWA KUJINYONGA, AMEAGA STATUS KWA PICHA YAKE YA ZAMANI
Mwanachuo wa Uhasibu TIA mkoani Mtwara anayefahamika kwa jina moja la Reagan amejinyonga kwa kujiua ikihisiwa ni baada ya ugomvi na mpenzi.
Mwili wa Reagan aliyekua akiishi mtaa wa Chikongola Mikindani umekutwa ukining'inia chumbani kwake Jana July 4, 2023.
Baadhi ya mashuhuda wamesema,
" Huenda Reagan aliamua kujiua kisa mapenzi kwasababu siku sio nyingi aligombana na mpenzi wake waliyekua wanaishi pamoja."
Kamanda wa polisi Mtwara Nicodemus Katembo amethibitisha kupokea taarifa za tukio hilo na kusema atalitolea ufafanuzi
baada ya ripoti ya uchunguzi wa madaktari kukamilika.
Mwili wa Reagan umehifadhiwa hospitali ya rufaa ya mkoa ya Ligula.
Muda mfupi kabla ya marehemu Reagan kujinyonga aliweka ujumbe whatsapp status akiuambatanisha na picha yake ya utotoni uliosomeka 'kwa jasho lako utajipatia chakula hadi utakaporejea mavumbini ulimotwaliwa, MAANA WEWE NI MAVUMBI NA MAVUMBINI UTAREJEA'.
Nifollow instagram @vivimachangeblog
Tangaza hapa wasiliana nami kwa 0755200023
CHEKA
Utakaa hivi ikiwa unamuendesha mama mkwe?๐คฃ
Tangaza Biashara yako hapa wasiliana nami kwa 0755200023
Nifollow instagram @vivimachangeblog
Mama mkwe wa Beyonce “ameoa”
Gloria Carter mama mzazi wa rapper mkongwe Jay-Z amemuoa mpenzi wake wa muda mrefu mwanadada Roxanne Wilshire jumamosi iliyopita jijini New York nchini Marekani.
Miongoni mwa waliohudhuria harusi hiyo ni mwali wake Beyonce , mjukuu wake Blue Ivy ambaye ni mtoto wa kwanza wa Beyonce na Jay-Z pamoja na mama wa Beyonce Tina Knowles Lawson.
Gloria amejaliwa kuzaa watoto wanne wakubwa wa kiume kabla hajajitangaza kuwa ni msagaji.
Tokea ajitangaze kuwa ni mpenzi wa jinsia moja mwanae bilionea Jay-Z amemuunga mkono mama yake kwa asilimia 100.
Nifollow Instagram @vivimachangeblog
Subscribe to:
Posts (Atom)