Tuesday, July 11, 2023

WALIO KISS MOI

Juzi jumapili julai 9, 2023 mchana video ilisambaa mitandaoni ya mgonjwa aliyekua amelazwa wodini katika hospitali ya Muhimbili akila denda na mwanamke.

Menejimenti ya Tiba ya Mifupa ya hospitali hiyo MOI imetoa ufafanuzi kuhusu uvunjifu wa maadili ya Kitanzania uliofanywa na mgonjwa huyo jina limehifadhiwa aliyekua amelazwa wodi namba 3A.

Mgonjwa amekiri kufanya kitendo hicho na mwanamke aliyedai ni mpenzi wake.

Kama ilivyodhaniwa na wengi wa waliotazama video hiyo ya kwamba mwanamke huyo ni muuguzi; MOI imebaini sio muuguzi wala mfanyakazi wa MOI na kwamba video ilirekodiwa na mgonjwa wa pembeni na tendo la denda kuendelea lilikatishwa na muuguzi wa zamu.

MOI inalaani na kukemea kitendo cha kurekodi video wodini na kuisambaza mitandaoni pia kitendo mgonjwa aliyekula denda kuvunja maadili ya Mtanzania kwani ni kinyume na miongozo ya wizara ya afya.

Aidha mgonjwa huyo pia
amewaomba msamaha Watanzania.



NiFollow instagram @vivimachangeblog

Kwa MATANGAZO ya Biashara nicheki 0755200023


No comments:

Post a Comment