Pages

Monday, February 29, 2016

SANDALS ZA KISIGINO ZA NGOZI NA SHANGA

Hivi viatu ni member mpya kwenye collection yangu.Viko vichache, kama unahitaji nijulishe 0755 200023



WEKA COVER DIRISHANI KWA AJILI YA KUZUIA MWANGA UNAOKERA USINGIZI WAKO


Mwanga wa asubuhi chumbaniunaweza kuwa kero hasa pale ambapo bado sio muda wako wa kuamka. Ili kuondokana na kadhia hii weka cover za maridishani wakati wa kulala. Uzuri wa cover hizi ni kwamba hazina mikunjo/marinda kama pazia kwa hivyo hata gharama yake iko chini. Endapo unahitaji tuwasiliane unipe size ya dirisha lako. 

Upambaji wa nyumba za tofali za gharama nafuu

Kuna baadhi ya watu wanaogopa kuwa huenda wasiweze kupamba nyumba zao kwa namna wanayotaka endapo wataamua kujenga kwa kutumia tofali za gharama nafuu. Nyumba za kisasa za gharama nafuu ni  zile zinazojengwa kwa tofali za gharama nafuu za kupishanisha za hydraform.

Emmanuel Adauth ambaye ni

Friday, February 26, 2016

VMC:.....Table mats za mkeka za nailoni

Table mats zinasaidia kuzuia meza isipate madoa ya michuzi na pia isikwaruzwe na vyombo wakati wa kula. 

Table mats za mkeka wa nailoni kifurushi cha pisi 6 sasa zinapatikana kwa umbo la duara na pembe nne. 



Endapo unahitaji karibu 'wasap' 
0755 200023

nifuate ig @vivimachangehomes

Thursday, February 25, 2016

VMC:... Carpets za watoto zenye alphabets..... zaidi ya kukalia pia anajifunzia

Carpet lina herufi  zote za alphabet mbele na nyumba
Michoro mingine ya kuwezesha kujenga iq ya mtoto mapema pia ipo
Hey wapenzi, carpet za watoto za kuwawezesha kujifunzia sasa zinapatikana. Ni za plastiki kwahivyo zaidi ya wepesi wa utunzaji hakuna cha wasiwasi wa vumbi kumletea mtoto mafua. Size ni upana wa mita moja na nusu kwa urefu wa mita moja na centimeter 80.

Endapo unahitaji karibu 'wasap' 0755 200023

VIVI MACHANGE HOMES: Project ya kuboresha bustani

Project yangu ya sasa ni maboresho ya hii bustani. Nasubiri kwa hamu kuona matokeo mwenye nyumba anayotaka. Rafiki, je una popote panapokutatiza kuhusu muonekano wa nyumbani kwako? Nitakushauri utapata uelewa na nitakuunganisha na watu wa kukufanyia kazi yako na mwishoni utapata matokeo unayotaka tena kwa gharama nafuu mno. Karibu
Kilicho kizuri tunakiendeleza na palipopwaya tunapafanya pawe pazuri. Kwa mfano haya magimbi yanapendeza sana lakini angalia zile canadian grass kule chini zinakufa kwakuwa zimezidiwa kivuli.

Palm linapendeza ila tutaliongezea maua ya rangirangi kupunguza kijani.
Garden entrance inavutia ila tutaiongezea maua iwe na muonekano wa kibustani zaidi.

PICHA: Matumizi mazuri ya kona

Nimekutana na hii picha nikaipenda kuhusu huu ubunifu wa kutumia kona kwa ajili ya kuweka mashelfu ya vitabu. Unapopamba angalia uwezekano wa kutumia vizuri nafasi zote zilizopo. Bila shaka matumizi haya ya kona ni mazuri.

Wednesday, February 24, 2016

PICHA: Hili duka lina taa nzuri za mezani

Nimevutiwa na background ya hii picha. Angalia zile taa za mezani za designs na rangi mbalimbali, hakika nimependa inabidi nipatembelee. Kama una taa za mezani nyumbani kwako tafadhali nitumie picha huenda zikasaidia kuelimisha wengine. Ukishea ujuzi unajisikia vizuri.

ni follow ig @vivimachangehomes

Tuesday, February 23, 2016

BONDIA MANNY PAQUIAO AWAJENGEA NYUMBA 1000 WASIOJIWEZA


Bondi wa Kifilipino wa Uzito wa juu Duniani, Manny Paquiao, amemaliza awamu ya kwanza ya ujenzi wa nyumba za kisasa kwa watu wasiojiweza katika eneo alilokulia liitwalo Sarangani.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Paquiao ameandika kuwa tayari amefanikiwa kumaliza nyumba kwa ajili ya maelfu ya familia katika mpango huo kwa awamu ya kwanza.

“I’m so happy giving this houses free to my constituents in Sarangani Province from my own pocket more than thousand families are the beneficiaries. and i’m still building more because i always believe what the bible says; 1 Peter 4:8-10 NIV
[8] Above all, love each other deeply, because love covers over a multitude of sins. [9] Offer hospitality to one another without grumbling. [10] Each of you should use whatever gift you have received to serve others, as faithful stewards of God’s grace in its various forms. Thank you Lord for everything even some people are criticizing me but I’m still happy because you live in me.” Ameandika.


Wiki iliyopita kampuni ya mavazi ya kimichezo ya Nike, ilisitisha mkataba wa udhamini na bondia huyu baada ya kuwafananisha wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja na wanyama.

ni follow ig @vivimachangehomes

Monday, February 22, 2016

Namna ya kukabiliana na changamoto ya kusambaa midoli ndani ya nyumba

Je wewe ni mzazi na una lundo la midoli kila mahali kwenye nyumba yako? Kama unahisi swali hili linakugusa basi sio wewe peke yako mwenye changamoto hii. Ni asili kwa mzazi kupenda kumnunulia mwanae midoli na michezo mbalimbali ya kidigitali na elektroniki inayoendana na wakati, na hasa kwenye siku ya kuzaliwa au sikukuu ndipo inakuwa mingi zaidi.

Nimeshuhudia nyumba zenye watoto ambapo midoli na

VMC:....PAZIA NZURI IMARA NA BEI NAFUU

Hey wapenzi, 
Kama kawaida yangu ya kukuletea vitu vizuri, imara na kwa bei utakayoimudu; hapa nakuletea pazia kwa gharama nafuu kabisa. Upana ni mita 2 na urefu ni mita 3, ni nzito na bei yake ni elfu 35. 
Kama unahitaji tuwasiliane 0755 
200023




Ni follow instagram @vivimachangehomes

Fahamu aina za urembo wa kisasa wa nguzo za nyumba


Nguzo za nyumba ni sehemu ya fahari ya usanifu wa nyumba ambapo zinaweza kuwa ni kwa matumizi au ni kwa mapambo tu. Kuweka nguzo ndani na nje ya nyumba imekuwa ni njia mojawapi ya kufanya muonekano wa nyumba uvutie zaidi. Katika historia ya ujenzi, wahandisi na wasanifu wamekuwa wakibuni njia za kuongeza mvuto kwenye majengo. Nguzo zimekuwa zikitumika kuleta muonekano wa kifahari ndani na nje ya nyumba za kisasa na zinaweza kuwepo kwenye chumba chochote, japo zinapendeza zaidi kwenye

Sunday, February 21, 2016

VIVI MACHANGE HOMES: Project ya Kumshauri Mwenyenyumba Kuhusu Bustani za Kuzunguka Nje na Ndani ya Fence

Hey friends,
 Natumai jumapili inamalizika salama. Hii ni project yangu kwa sasa ambapo mteja anataka ushauri wa mitindo ya bustani za kuzunguka fence kwa nje na ndani. Habari ninayotaka ujue ni kwamba mteja wangu huyu yuko mkoani, kwahivyo huwa nafanya ushauri wa onsite na offsite. Kushauriana ni kuzuri wapenzi. Kama uko mbali nitakutumia picha nitakupa maelezo, tutajadiliana na utauliza lolote linalokutatiza na kwa muda wowote hadi upate unachokitaka. Na gharama yangu nakuchaji mara moja tu hadi kazi yako iishe..karibu
Hii ndio nyumba mwenye nayo anataka ushauri juu ya kuotesha bustani za kuzunguka hii fence kwa nje na kwa ndani. Uzuri wangu ni kuwa nakushauri, unaelewa nawe unakuwa mtaalam unaenda kufanya kazi yako mwenyewe kwa kumuelekeza kijana na bustani. Maana yake ni kwamba una save hela nyingi badala ya ungemuajiri landscaper/gardener...kwanini upoteze hela nyingi? Pata ujuzi kisha fanya mwenyewe!

Kwa ndani eneo la kona unaweza kutengeneza kitu kama hiki na ukaotesha kichaka chake cha maua, ukapata na kiukuta cha kukalia

kama kiukuta ni gharama basi tupia mawe na mimea namna hii.

Unaweza kuamua kuzungusha ukutani yale majani ya kutambaa, naamini ulishawahi kuyaona. Ukifanya hivyo kupiga ukuta  rangi tena ndio kwaheri.

Kwenye kona unaweza kuotesha maua mchanganyoko na eneo lingine ukaotesha boda ndefu.

Pia unaweza ukaacha udongo wazi kuonyesha mwisho wa ukoka kama hivi.

Ukiotesha hivi kwa nje inavutia.

Thursday, February 18, 2016

NYINGINE TOKA COLLECTION YANGU (VMC):....Mito Flat


Hey friends,
Hii mito flat ni ongezeko jipya kwenye VMC. Size ni inch 20 kwa 20 inafaa kukalia chini, kwenye gari, ofsini na kwenye viti vya chuma au plastic. Pia inafaa sana kwa wajawazito. 

Inasaidia kuongeza mguso wa rangi mahali; rangi zilizopo ni orange na nyekundu. Inanunulika kwa kasi kwahivyo kama unahitaji nijulishe fasta..0755200023

Wednesday, February 17, 2016

KUTOK KWANGU:...Dondoo za maandalizi ya kupamba nyumba yako


Kupamba nyumba inaweza kuwa kazi ngumu na ya muda mrefu kwa baadhi, ingawa pia wapo wanaoona ni kazi ya kuvutia na wanaifurahia. Haijalishi wewe uko kwenye kundi gani lakini ni kwamba inaweza kukuchukua miezi kupata pambo dogo tu kama vile picha unazotaka kutundika ukutani ambazo unaamini utazipenda kuziangalia kila siku. Ukweli ni kwamba vitu vya nyumbani vimetawanyika kwenye masoko mbalimbali na vingine ni vidogodogo kiasi kwamba vinachukua muda mrefu kuvikusanya pamoja. Na vilevile inategemea na kipaumbele cha mwenye nyumba kwamba ni nini anataka kwa uwezo na umuhimu wa kuwa nacho kwanza kabla ya kingine.
Kwahivyo kazi ya kupamba inaweza kuwa ni ya kudumu au laa ikachukua muda mrefu tu.

Mambo matatu muhimu sana katika

PICHA: PATA IDEAS YA SEHEMU MBALIMBALI UNAZOWEZA KUWEKA VIKABATI VYEMBAMBA/SIDEBOARDS

Uki google neno sideboards utaona aina mbalimbali za hivi vikabati vyembamba.

Unaweza kuweka kikabati chembamba kwenye corridor endapo corridor yako ni pana. Zaidi ya mvuto pia kinakuongezea sehemu ya hukifadhia kwahivyo nyumba kuwa na mpangilio.
Vikabati vyembamba pia vinaweza kuwa bafuni chini ya sink na humo unahifadhia vitu mbalimbali kama vile tissue na dawa/sabuni za kusafishia.
Kikabati chembachmba pia unaweza kukiweka kwenye baa ya nyumbani. Kuna wenye nyumba ambao wana varanda zilizozibwa (aidha kwa grill) na pia wengine wana nyumba za ghorofa na wanapenda kuweka eneo la bar pale kwenye balcony. Kama unalo eneo kama hilo basi waweza weka kikabati chembamba/sideboard

Kikabati chembachea pia waweza kukiweka kwenye dining room. Juu ya kikabati panasaidia kama sehemu ya kuwekea mabakuli ya vyakula kabla ya kuanza ku serve na ndani unahifadhi vyombo vya kulia.

Kikabati chembamba kinapendeza kwenye chumba chochote, hapa sebuleni kimehusika kama kabati la TV

Je una tatizo lolote kuhusu mapambo ya nyumba yako? Nijulishe 0755 200023

Nifuate instagram: vivimachangehomes

Monday, February 15, 2016

KUTOKA KWANGU:...Unavyoweza kuboresha fenicha za nje ya nyumba kwa kuongeza mito ya gharama nafuu

Huenda unapamba upya eneo la nje ya nyumba yako kwa kuboresha vilivyopo, bila shaka unataka kupata muonekano mpya ambao utaupenda bila kutumia gharama kubwa. Kwa kuwa na mito ya gharama nafuu unaweza kutengeneza muonekano wa kuvutia unaoutaka.

Nakupa dondoo hatua kwa hatua za njia rahisi za kukuwezesha kupata mito ya namna hiyo ili kuondoa ile ambayo imesinyaa au foronya zimepauka, zimechakaa au

PENDEZESHA NYUMBA YAKO KWA VITANDA VYA MBAO, PAZIA , MEZA ZA MNINGA NA SOFA ZA KISASA NA NZURI

Hello rafiki,
 katika kukidhi kiu yangu ya kuhakikisha kuwa nyumba yako inapendeza kwa gharama nafuu; nimeungana na Oiso ambao ni watengenezaji wa fenicha nyingi nzuri za ndani na kwa bei nafuu ambayo huwezi kuipata pengine popote (ukiipata pengine wee njoo nilalamikie). Tazama picha na bei na ukitaka kwa undani zaidi njoo "wasap" 0755 200023

Vitanda size 5 kwa 6 vya mbao za mninga bei ni mil 2



Sofa za seat 9 na mito yake bei ni mil 3.2...hapo wewe unaweza kutengenezewa kwa idadi ya seat unazotaka.
Dining table ya mninga ya watu 6 bei mil 1.9

Pazia nzito mita elfu 23 na nyepesi mita elfu 12. Fundi yuko anakushonea BILA gharama ya ziada.