Gloria Carter mama mzazi wa rapper mkongwe Jay-Z amemuoa mpenzi wake wa muda mrefu mwanadada Roxanne Wilshire jumamosi iliyopita jijini New York nchini Marekani.
Miongoni mwa waliohudhuria harusi hiyo ni mwali wake Beyonce , mjukuu wake Blue Ivy ambaye ni mtoto wa kwanza wa Beyonce na Jay-Z pamoja na mama wa Beyonce Tina Knowles Lawson.
Gloria amejaliwa kuzaa watoto wanne wakubwa wa kiume kabla hajajitangaza kuwa ni msagaji.
Tokea ajitangaze kuwa ni mpenzi wa jinsia moja mwanae bilionea Jay-Z amemuunga mkono mama yake kwa asilimia 100.
Nifollow Instagram @vivimachangeblog
No comments:
Post a Comment