Monday, July 24, 2023

MCHEKESHAJI JAYMONDY ANADAIWA KUMTELEKEZA MWANAE BAADA YA KUPATA GIRLFRIEND MZUNGU



Mchekeshaji #Jaymondy anadaiwa kutelekeza mtoto kisa kapata girlfriend mzungu.

Akieleza kwa uchungu mzazi mwenza wa mchekeshaji huyo amesema kipindi cha nyuma Jaymondy alikua anatoa matunzo ya mtoto na hata wao kama wazazi walikua na mawasiliano mazuri; lakini baada ya mzazi mwenzie huyo kupata mzungu mambo yamebadilika kabisa.


Baby mama huyo amesema mpasuko kati ya mzazi mwenzie na wao (mama na mtoto) ulianza kutokea baada ya Jaymondy kupata mzungu.
"Mapenzi yameisha kabisa kwa mtoto na hata hakumbuki ni lini kamjulia hali mtoto".
"Mtoto amefukuzwa shule ada na baba yake anaonekana mitandaoni akila raha Ulaya na hata alivyoondoka hakumuga mtoto", amesema baby mama wa Jaymondy.

Baby mama akaendelea kueleza kwa uchungu;

"Mzungu amefunga kila sekta hakuna mawasiliano kabisa."

Kwa sasa Jaymondy anaishi Scandinavia na mwanamke wake mzungu.

No comments:

Post a Comment