Wednesday, July 5, 2023

MWANAFUNZI WA UHASIBU MTWARA AMEJIUA KWA KUJINYONGA, AMEAGA STATUS KWA PICHA YAKE YA ZAMANI

Mwanachuo wa Uhasibu TIA mkoani Mtwara anayefahamika kwa jina moja la Reagan amejinyonga kwa kujiua ikihisiwa ni baada ya ugomvi na mpenzi.

Mwili wa Reagan aliyekua akiishi mtaa wa Chikongola Mikindani umekutwa ukining'inia chumbani kwake Jana July 4, 2023.

Baadhi ya mashuhuda wamesema,

" Huenda Reagan aliamua kujiua kisa mapenzi kwasababu siku sio nyingi aligombana na mpenzi wake waliyekua wanaishi pamoja."

Kamanda wa polisi Mtwara Nicodemus Katembo amethibitisha kupokea taarifa za tukio hilo na kusema atalitolea ufafanuzi
baada ya ripoti ya uchunguzi wa madaktari kukamilika.
Mwili wa Reagan umehifadhiwa hospitali ya rufaa ya mkoa ya Ligula.

Muda mfupi kabla ya marehemu Reagan kujinyonga aliweka ujumbe whatsapp status akiuambatanisha na picha yake ya utotoni uliosomeka 'kwa jasho lako utajipatia chakula hadi utakaporejea mavumbini ulimotwaliwa, MAANA WEWE NI MAVUMBI NA MAVUMBINI UTAREJEA'.

Nifollow instagram @vivimachangeblog

Tangaza hapa wasiliana nami kwa 0755200023

No comments:

Post a Comment