Saturday, November 14, 2015

PICHA: ULISHAWAHI KUFIKIRIA KUWA NA SAKAFU NYEUSI IWE NI TILES AU ZULIA?





Sakafu nyeusi naona kama inaonyesha ufahari na ukisasa...wee unaonaje? Sema nami..

Friday, November 13, 2015

PICHA ZA DRESSING TABLE KWA AJILI YA CHUMBA KIDOGO CHA KULALA

Wasichana wanapenda kuwa warembo na ndio maana hii fenicha inayoitwa dressing table ilivumbuliwa. Mdada anakuwa na kistuli, kioo na droo kadhaa za kuhifadhi vipodozi na vitupio vyake.

Dressing table ni sehemu muhimu katika chumba au bafu la mwanamke. Kila msichana au mwanamke anataka kuwa na eneo lake la kujidai, dressing table ni kona yetu ya urembo, kujipara, kupaka makeup na baadaye kutokelezea tukiwa tunajiamini. 

 Dressing table ya kisasa ikiwa na kila kitu cheupe
Droo za dressing table ni sehemu muhimu na rahisi ya kuhifadhia vipodozi, pafyum na vitupio. 
Kwahivyo wasichana, kama huna dressing table ya kisasa na kioo unatakiwa kununua au kutengenezesha moja ambapo itakusaidia kurahisha maisha yako ya chumbani. Chagua kona ambayo unaona inafaa na weka dressing table yako hapo. Hapo panaweza kuwa chumba cha kuvalia , cha kulala au bathroom kama kuna nafasi ya kutosha. 

Dressing table ni kwa kila kiumbe cha kike!
Kama unayo tayari, nishirikishe inakusaidia vipi na je uliipataje/uliinunua au kuitengenezesha wapi. Simu iko hapo juu..Asante kwa kunitembelea ..

Thursday, November 12, 2015

Vitu Vizuri-------DESIGNS ZA SOFA AMBAZO NI GIANT

Katika pitapita zangu za kukutafutia na kukuonyesha ni nini kipya cha kuifanya nyumba yako ipendeze zaidi nimekutana na haya masofa makubwamakubwa..Kusema ukweli yanapendeza na ni nani asiyetaka kukalia kochi la kunesanesa kwa mfano?
 Kwa wewe unayependa kuangalia luninga huku umelala, hapa unaweza kupotelea usingizini kabisa
Rangi wala isikutishe kwani ni velvet flani hivi inateleza na ina manyonya na hata ikishika uchafu ni rahisi sana kusafisha kwa povu la multipurpose cleaner
 Sofa murua kwa nyumba ya kisasa
 Hizi sofa kikukweli zinavutia. Kama una hela na unataka kubadili sofa, ukikutana na hizi hutaziacha.
 Sofa kubwa na comfortable kwa kukaa au kulala huku unaangalia TV
Kama kuna kipya cha nyumbani umekutana nacho tafadhali nijuze kwa simu au email hapo juu. Asante kwa kutembelea blog!

Wednesday, November 11, 2015

SKIRTING ZA TILES NI KWA MAPAMBO NA MATUMIZI

Skirting ni ule utepe mwembamba ukutani uwe ni wa rangi au tiles na huwa hili neno linatumika zaidi kwa sakafuni. Kwenye floor ya tiles skirting ya tile inatumika kulinda kile kisehemu kidogo cha ukuta mara utokapo sakafuni wakati kwa bafuni na jikoni skirting hiyo huweza kutumika kama urembo.
 Skirting za tiles zinakuja kwa style mbalimbali. Ukiona zenye rangi ya bluu inaashiria maji kwahivyo inatakiwa kuwekwa bafuni.
Tile za kawaida huwa hazina boarder. Kwahivyo mafundi wanatumia nguvu ya ziada kuzikata na kuzipamba ziendane na zile kubwa. Badala ya usumbufu huo na pengine ukosefu wa accuracy nunua boarder ambazo zimeshatengenezwa tayari kuendana na tile kuu.

Hii skirting yenye picha ya birika na vikombe inafaa kuchanganywa kwenye tile kuu za jikoni kama urembo

Tile kuu nyingi tayari zinakuwa na boarder zake zilizotengenezwa special ambazo unaweza kununua pembeni kuendana na design na rangi unayotaka


Zaidi ya kuchanganywa na tile kuu, hizi tiles za skirting zinaweza kutumika pekee kama decorations maeneo ya pembeni mwa ukuta wa kwenye ngazi na viambaza vya varanda.

Tuesday, November 10, 2015

NJIA 10 ZA KUWEKA MPANGILIO KWENYE CHUMBA KIDOGO CHA KULALA


1. Tandika kitanda. 
2. Hifadhi documents zote muhimu kwenye droo badala ya kuziacha zisambae kila mahali.

3. Tumia vizuri droo za pembeni mwa kitanda kuhifadhia, hii itakusaidia sana.

4. Hifadhi hereni bangili na vitupio sehemu moja maalum rahisi kuchukua na kutumia pale vinapohitajika. Ni ahueni kujua kila kitu na sehemu yake.

5. Chumba kidogo cha kulala kinamaanisha eneo finyu kwa kabati la nguo. Weka kitundikio rahisi . Pia ni pambo la chumba chako ukipendacho.
    Hifadhi waya na chaja za simu na kamera eneo moja. 

7.  Tumia ubao wa kutobolea documents zinazotakiwa kutendewa kazi karibuni kama vile bill ndogondogo na pia kumbukumbu za siku.

8.  Tumia vizuri kona za chumba. Mara nyingi huwa zinasahaulika. Unaweza kuweka vimeza kwenye kona na vikakupa eneo zaidi la kuhifadhia vitu kama vitabu mapambo na picha.

9. Kama bado unafikiri una vitu vingi basi tumia mvungu wa kitanda. Droo za mvunguni ni nzuri kuhifadhia vitu kama shuka na mataulo.
10. Unakumbuka wakati ilikuwa sawa kuweka picha ukutani kwa kutumia tape? Nyakati hizo zimeisha. Tumia vitundikio maalum vya picha za ukutani na itasaidia kuondoa hali ya mrundikano.



Monday, November 9, 2015

PICHA: Meza Zenye Top ya Marble Lakini Miguu ya Mbao


Meza hizi zina top ya marble lakini miguu ni ya mbao. Kuamua full marble au mix inategemea na personal taste. Je, wewe mdau unapendelea ya full marble au mix kama hii? Binafsi hii ya mix nimeipenda zaidi inaonyesha elegance fulani hivi amaizing..

Friday, November 6, 2015

KUPAMBA KWA VIOO

Haijalishi umekiweka wapi kioo cha mapambo ni njia mojawapo ya kuakisi mwanga na kufanya chumba kionekane kikubwa
Bila kujali ukubwa wake, kioo ni njia mojawapo ya kuonyesha unadhifu wa chumba
Kioo sio bestie wa bafuni tuu hata dining kinahusu

Kioo kinalipa jicho kitovu cha chumba

Gallery ya vioo badala ya picha..

Wednesday, November 4, 2015

TREND 6 ZA MASINKI YA KISASA YA BAFUNI YALIYOPO KWENYE CHATI BONGO

Ile tabia ya kwenda kwenye duka la vifaa vya ujenzi na kutafuta sinki nyeupe kwa ajili ya bafuni inapitwa na wakati. Sasa sinki za kisasa za bafuni zinakuja kwa rangi mbalimbali na zina kabati ya kuhifadhia chini yake. Sinki aina hii linatokeza juu ya kaunta
 Sinki hili limezama chini ya kaunta na linasimama na miguu yake
Sinki hili linasimikwa ukutani na halina  miguu

Hili lina mvuto wa kipekee. Ni kama bakuli limewekwa tuu chini ya bomba
Kama unataka muonekano wa mbao basi sinki hili linakufaa zaidi

PICHA: CARPET LA IKULU

Maalim Seif na Raisi Kikwete wakiteta jambo. Mi naangalia hili carpet, hivi akija mkaaji mwingine analibadilisha eti..

Tuesday, November 3, 2015

FAIDA ZA KUPAMBA UKUTA KWA WALLPAPER NI HIZI

Kuna faida nyingi za kutumia wallpaper badala ya rangi kwenye ukuta wa nyumbani. Faida moja kuu ni kuwa wallpaper zina michoro, rangi na style mbalimbali.

Wallpaper zinakupa fursa ya kuibandika upande wa ukuta unaotaka. Kwa mfano hapa ukuta wa kushoto una rangi kuoanisha na hiyo vesi mezani, wakati ukuta wa mbele una wallpaper

wallpaper ziko za pattern rangi na designs lukuki

Wallpaper ni rahisi kusafisha kwa maji

Wakati rangi unaweza kupaka kila baada ya miaka miwili, wallpapers zinadumu kati ya miaka 10 hadi 15

Wallpaper kwenye ukuta wa tendego bedroom

Baadhi wa wallpaper unaweza kuzipaka rangi. Pia usimikaji wa wallpaper ni rahisi na hauchafui kama kupaka rangi, tuseme labda nyumba tayari imeshaanza kutumika.

Monday, November 2, 2015

MEZA HIZI ZA MARBLE BILA SHAKA ZITAKUFANYA USAHAU MBAO

Mbali na marble kuwa mailighafi ya sakafu na ujenzi, kwa siku za karibuni inakuja kwa kasi kwenye kutengenezea meza. Meza za marble naturally zina uzuri wa asili hazihitaji pambo la ziada.


Ni muhimu kutumia na coaster au mart ili kusitokee mikwaruzo

 Zaidi ya uzuri wake, meza za marble hazipitwi na fashion na pia ni imara sana
Ziko za style na michoro mbalimbali

Sunday, November 1, 2015

Box za pazia zina faida kuliko fimbo za pazia

Kwa siku za karibuni watu wengi wamekuwa wakifunga fimbo za pazia kuliko ya box za pazia. Pengine ni urahisi wa kupatikana kwake kwakuwa zipo za aina na mitindo mingi. Ila ukiangalia kiundani box za pazia zina faida zaidi.

Juu ya box za pazia unaweza kusimamisha fremu za picha ambapo kwenye fimbo za pazia haiwezekani.
Box za pazia zinaongeza urembo wa pazia.

Kwa leo nimeongelea box za pazia, mbeleni nitaongelea fimbo za pazia.