Saturday, October 31, 2015

----vitu vizuri----VYUNGU VIKUBWA VYA MAUA VYA NDANI YA NYUMBA

Vyungu vya kisasa vya maua kwa ajili ya ndani vimekuwa vyenyewe ni pambo tayari, bila hata maua kuweko nadani yake. Hebu angalia picha
Vipo vyungu vya maumbo urembo na rangi mbalimbali. Chagua kuendana na decorations nyingine zilizopo ndani ya nyumba unayoishi.



Saturday, October 24, 2015

Makabati ya Kisasa ya Nguo

Kabati la nguo ni muhimu kwa uhifadhi wa nguo uliotukuka vinginevyo ni kusababisha mrundikano na utunzaji wa nguo usiofaa. Kama hauna kabati la nguo lililojengewa ukutani basi bila shaka makabati haya ambayo ni free standing mojawapo litakufaa. Angalia picha
 Handle zake ni kubwa vizuri. partition zote zipo ndani ndio maana halina droo
 Hapa ni mwendo wa funguo endapo unataka kuloki pia droo za ziada chini

 Hili pia handle zake ni kubwa vizuri
Kama vipi ongeza droo za ziada

Thursday, October 22, 2015

Rangi 8 za Kipekee za Nyumba Zilizopo Kwenye Chati kwa Sasa

Rangi za kipekee kwa sasa kwa ajili ya kupaka nyumba ni hizi tunasema rangi za rafu yani rough paints. Tukubaliane kuwa rangi hizi unaweza kupaka kuta maalum tu kama si nyumba nzima.
Tazama picha ujionee mwenyewe..
Hii inaitwa ngozi ya tembo. Ni ya kupaka maeneo kama vile ya kwenye nguzo
Kitu cha lime green


Kama kitambaa cha nguo vile

 Licha ya kwamba zinapendeza kwa sanaa yake ni kuwa pia zinaficha ubovu wa ukuta usio smooth.
Inafaa jikoni hasa ule ukuta wa kutenganisha na dining

Kitu cha kung'aang'aa


Wednesday, October 21, 2015

BIZARRE: Amber Rose akiwa amepozi uchi kwenye jarida la GQ

She certainly looked amazing in the photo, which showed her wearing nothing but a pair of high heels

Picha: Wanasayansi wametengeneza jibwa la kutisha

Huyu ukiwa naye nyumbani bila shaka bajeti yake itakuwa sawa na ya familia..loo

Scientists have created a new breed of stronger, faster dogs using DNA manipulation


Faida za kuwa na kioo juu ya meza ya chakula ya mbao


Meza ya chakula sio tu sehemu ya kukutana familia na marafiki wakati wa chakula, bali pia ni fenicha kubwa yenye kuhusika na muonekano wa ndani. Kama umeshanunua moja au labda unayo tayari bila shaka utakuwa nayo maisha yako yote. Kwahivyo fanya kila uwezalo ili kuiwezesha ivutie na idumu miaka mingi.

Pamoja na kuwepo kwa meza za

Tuesday, October 20, 2015

---Vitu Vizuri----Dining Table za Kisasa za Cleopatra sasa zipo Dar

Bila kumung'unya maneno ni kwamba meza za kulia chakula za Cleopatra zina uzuri mithili ya jumba la mfalme na malkia. Natumai ulishawahi kusikia kuhusu huyu mwanamke Cleopatra ambaye alikuwa na uzuri wa kutisha na inasemekana duniani hajawahi kutokea mzuri tena kama yeye.

Finishing zake ni za sanaa ya kutisha kwa uzuri na umakini uliotumika. Zina asili ya Egypt

Zimetengenezwa kwa mbao ngumu na sio maboksi ya kichina. Kwanini upigizane kelele na fundi. Ukiwa na meza hii hutajutia hela yako maisha yako yote.

Juu ya meza kuna kioo maalumu chenye unene wa kutosha kiasi kwamba hata ukikikalia hakivunjiki. Kila kioo ni maalum kwa meza yake.

Hebu angalia huo urembo uko hadi mvunguni kwenye miguu ya meza.

Hizi meza ni imara na zina uzuri wa kutisha. Ukiiweka ndani lazima dining room yako itakuwa na hadhi ya presidential. Nenda leo kawaone na ukiwaambia Vivi amekutuma utapewa discount.

Pia unaweza kuwafuata kwenye account zao ambazo facebook ni cleopatraTZ wakati twitter ni cleopatra_tz na instagram ni cleopatratz

Monday, October 19, 2015

UREMBO WA NGUZO WA KISASA AINA YA MOSAIC

Zaidi ya mawe ya asili kama yale ya Tanga, basi unaweza kurembesha nguzo za nyumba yako kwa kutumia vitaili vidogo dogo vinavoitwa mosaic. Twende pamoja utizame picha za aina mbalimbali za mosaic

Add caption







Sunday, October 18, 2015

Inasikitisha nyumba ya Mheshimiwa Mbatia yaungua

Kwa mujibu wa taarifa za habari ni kwamba nyumba ya Mheshimiwa Mbatia imeungua kutokana na umeme mkubwa. Hii inatukumbusha wenye nyumba umuhimu wa kukatia insurrance nyumba zetu kwani chochote kinaweza kutokea. Pole sana Mbatia

Saturday, October 17, 2015

Picha ya nyumba ya marehemu Mheshimiwa Deo Filikunjombe

Haya ni makazi ya aliyekuwa mbunge wa Ludewa yaliyopo eneo la Kijichi
Dar es Salaa. bila shaka msanifu wa hili jengo aliitendea haki taaluma yake. Pumzika kwa amani mheshimiwa Filikunjombe

Mabembea ya kisasa


Mambo yanabadilika kila uchao. Sasa hata ukiamua kuweka bembea bedroom inawezekana. Bembea za kisasa kama hizi zinahamishika na ukaziweka popote, huna haja tena ya cement na zege. Mungu atupe nini tena kipindi hiki wanadamu wenzangu kila kitu kipo ni pesa yako tu..

Friday, October 16, 2015

Mitindo mitano ya masinki ya kisasa ya jikoni

Mtindo au muundo wa sinki la jikoni ni muhimu uendane na ukubwa na matumizi ya jiko. Ifuatayo ni miundo mitano ya masinki ya jikoni na matumizi yake
Hili sinki ni kubwa lakini lina karai moja na sehemu ya kuwekea trey la kukaushia vyombo. 
Sinki hili ni dogo kuliko yote na lina sehemu ya karai peke yake. Hili linafaa zaidi  kwa jiko la mtu mmoja au wawili tu
Hili sinki ni dogo lakini lina karai moja na sehemu ya kuwekea trey la kukaushia vyombo. 


Sinki hili lina makarai mawili moja kubwa na kingine kidogo pia kuna sehemu ya trei. Hili ni kwa jiko la saizi ya kati kwa matumizi ya watu watano
Sinki hili lina makarai mawili makubwa yenye ukubwa unaolingana. Mtindo huu ni sahihi kwa jiko kubwa na ingekuwa mimi kati ya mitindo yote mitano ningechagua huu

Thursday, October 15, 2015

Designs mbalimbali za vitanda vya kisasa vilivyopo bongoland

Kama vip bora ukadunduliza lakini ukanunua kitanda cha ukweli

Kitanda cha pink malkia wa bedroom

 Comforter limetandikwa likaitika. Kwa picha zaidi zama "read more"

Wednesday, October 14, 2015

Namna ya kuleta mvuto getini




Hapo kwenye lango kuu la kuingilia nyumbani kwako almaarufu getini bila shaka ndio mbele ya nyumba yako. Ni eneo ambalo mgeni wako anapata hisia za mwanzo kabisa juu ya nyumba yako, kwa hivyo pafanye pavutie. Elimika kwa dondoo hizi za namna ya kuongeza mvuto kwenye eneo la mbele la lango kuu kwa kuboresha kile kilichopo na kuondoa muonekano wa nyumba iliyochoka:

·       Weka paa juu ya geti. Paa juu ya geti lina faida kama pambo na matumizi vilevile.

Vitu vizuri.....Picha za vyumba vya mtoto wa mbelezzz

Angalia hizi picha za vyumba mbalimbali vya mtoto ndani ya nyumba moja. Japo ni mbelezzz lakini hata wewe ukiamua unaweza. Roho yako tu ipende...
Hapa motokaa zimehifadhiwa zikatulia tulii



Sebule ya mtoto

Treni hiyoo hadi Kigomaa