Sunday, April 30, 2017

Blauzi za shifoni na za kiutamaduni zipo

25,000
Top hizi za culture ni free size




22,000

Blauzi za shifoni zenye vifungo mbele hadi kifuani zipo size Medium, Large na XL.

Zinapatikana kwa jumla na rejareja kwako wewe unayetaka kuvaa au wewe unayetaka kwenda kuuza.
0755 200023

Friday, April 28, 2017

Blauzi za shifoni zipo

Top hii ya shifoni ina kitabaa kingine cha ndani (lining) cha shifoni pia. Kwa wadada wanaojipenda kwa ajili ya kuvalia jeans,tight na sketi za kuendea kazini.
Kwa saizi na bei click kwenye vinavyozwa. jumla na rejareja zipo za kutosha
0755 200023

Haya magauni mawili ndiyo yaliyouzika zaidi

Haya magauni mawili ndio best seller so far. Yapo hadi XXL, zawadi sahihi kwa mother's day
0755 200023

Wednesday, April 26, 2017

Gauni hili linafaa kanisani au harusini

Gauni hili naliita ni la mdada wa heshima anayeenda sehemu aheshimike kutokana na muonekano wake. Linafaa kuvaliwa kanisani, harusini na kadhalika. Kitambaa chake ni cha lace iliyojishikilia humohumo. Yaani haina vitambaa viwili. Kulinunua bonyeza kwenye vinavyouzwa. Simu 0755 200023

Gauni fupi la lace. Nguo zote ni chini ya elfu 41. Bonyeza kwenye Vinavyouzwa

Lace mini dress. Rangi zilizopo ni peach na nyeupe. Size 46, 48 na 52. Bei 40,000
0755 200023

Friday, April 21, 2017

Namna ya kuchagua mtindo wa wallpaper

 
Tunaweza kusema kuwa wallpaper ndio habari ya mjini kwa sasa kwa ajili ya kupendezesha vyumbani kwenye nyumba nyingi za kisasa hasa  sebule. Tatizo lililopo ni changamoto ya mtindo upi ndio sahih kutokana na uwepo wa wallpaper za rangi na michoro mingi mno. Hadi zile flati yaani zisizo na mchoro wowote.

Elimika na dondoo hizi za namna mnunuzi anayetaka kupamba kwa

Wednesday, April 5, 2017

Maandalizi ya ukuta kabla ya kubandika wallpaper



Wanasema kila safari moja kubwa inaanza na hatua moja ndogo. Na hata katika swala la kubandika karatasi za kupendezesha kuta zijulikanazo kama wallpaper, hatua ya mwanzo ndio yenye umuhimu mkubwa. Wallpaper hazishiki au kudumu kwenye kuta zenye mafuta, chafu au rangi inayobanduka. Na ndio maana siwezi kuchoka kusisitiza ni kwa kiasi gani ni muhimu kuandaa kuta vyema kwa ajili ya ubandikaji wa wallpaper.

Kwa kuta zilizopakwa rangi zamani
Hizi ni zile kuta za zamani, yaani nyumba ambazo zilishapakwa rangi kitambo na tayari watu wanaishi.
Endapo lengo ni kubandika wallpaper kwenye kuta za aina hii hazitakiwi kuwa na rangi zilizobanduka na wala maeneo yenye vinundunundu, nyufa au vishimo. Endapo maeneno hayo yapo inabidi kuyaondoa kwa kukwangua na kurekebisha kwa kufuata hatua kama zile za uandaaji kuta wakati unapotaka kupaka rangi ila unaishia kwenye hatua ya primer ambayo huwa ni ya mwisho kabla ya kuanza kupaka rangi yenyewe. Kwa maana hiyo panatakiwa pawe nyororo kabisa. Baada ya hapo ukuta wote usafishwe kwa sponji au kitambaa kilicholoa ili kuondoa vumbi. Mara ukuta huu unapokuwa umekauka ndipo ubandikaji wa wallpaper unapoweza kuchukua hatua.

Kwa kuta zenye wallpaper ya zamani
Kuta nyingi ni rahisi kufanyiwa maandalizi kuliko ambazo zilikuwa na wallpaper tayari na unataka kuibandua ili kubandika mpya. Kwanza kabisa ni vyema ufahamu kuwa ni lazima uondoe kwanza ile ya zamani. Mafundi wengi wanaobandika wallpaper wanajua pia jinsi ya kubandua.

Kuta zenye ukungu
Ukungu unaweza kuonekana kwenye kuta kwa rangi ya njano, kijani, kijivu au nyeusi. Kama hali hii ipo kwenye ukuta unaotaka kubandikwa wallpaper paoshe kwanza kwa maji ya moto yenye blichi. Paache pakauke kabisa halafu papake primer kabla ya kubandika wallpaper. Pakishabandikwa wallpaper ukungu hauwezi kuota tena kwani wallpaper zilivyotengenezwa haziruhusu ukungu kuota juu yake.

Kuta mpya
Endapo kuta/nyumba ni mpya na umefikia kwenye hatua ya kupaka primer (kama tulivyosema huko juu katika maandaliza ya kupaka kuta rangi) unachotakiwa ni kuepuka gharama mara mbili za kupaka ukuta rangi ya mwisho halafu wakati huohuo unataka tena kubandika wallpaper juu yake.  Badala yake unachotakiwa ni kuishia kwenye ngazi ya primer tu kwenye ukuta wowote unaotaka kubandika wallpaper halafu badala ya ngazi inafuata ambayo ni ya mwisho yaani kupaka rangi ndipo unabandika wallpaper.

Natumai msomaji wangu umeelewa vizuri kabisa namna ya kuandaa kuta za aina mbalimbali endapo unataka kuzibandika wallpaper. 

Tunazo wallpaper za michoro zaidi ya 100. Wasiliana nasi kwa namba 0755 200023

VITANDA, MEZA YA CHAKULA NA KABATI LA VYOMBO VIPO

Kitanda 6 kwa 6 bei ni 1.3m

Meza ya chakula ya watu 6 bei 1.3m

Kabati la vyombo very classy 1.2m

Kitanda 5 kwa 6 bei ni 1.2m

Mawasiliano kwa biashara tu ni
0755 200023