Friday, July 16, 2021

HATUA ZA KUTATUA TATIZO ILI UBAKI NA HESHIMA YAKO

 Follow Instagram |@vivinavisavyake

Ukipatwa na tatizo kama unataka ulitatue kwa jinsi ambayo mwishoni utabaki na heshima yako basi fuata hatua hizi.

1. Unapolipokea usihamaki bali lijue tatizo kwa undani na kwa ukweli
2. Fahamu unachotaka kutokana na hilo tatizo.
3. Angalia mifumo iliyopo na uchague utakaoweza kutatua tatizo lako.
4.Fuatilia mfumo uliochagua je unatatua ama unaongeza tatizo.
5. Kama mfumo uliochagua unatatua basi utakupatia suluhisho na kama hautatui badilisha chagua mwingine.
6. Anza kutekeleza suluhisho.

Pia kwa undani zaidi unaweza kufuatilia you tube search Vivi Na Visa Vyake

Thursday, May 6, 2021

NAMNA YA KUEPUKA WIVU

 FOLLOW Instagram @vivinavisa vyake


Ili uweze kuwa na mahusiano mazuri ni lazima ujifunze namna ya kuepuka wivu. 

Kila mtu ameumbwa na wivu tofauti kati ya muonekano wa wivu wa mmoja na mwingine ni ninsi unayemdani hana wivu anavyoweza kuukabili wivu wake na yule unayemuona ana wivu ni jinsi asivyweza kuukabili wivu wake.

Hivyo basi ili kuepuka kuonyesha kiwango cha wivu wajo waziwazi ili hatimaye uwe na furaha na pia na mahusiano mazuri na watu inabidi ufanye yafuatayo:
1. Usijilinganishe na safari ya mwingine maana kila mtu bhapa duniani ana safari yake ya kipekee.
2. Huenda hauko kwenye hatua kama ya unaowaonea wivu kwa ajili |Mungu amekupangia kuna jema lako linakusubiri
3. Muonekano wa wengine unaweza kuona ni mrahisi kumbe hujui stori yao yote.
4. Epuka kufuatilia ya wenzingine maana kunaweza kukuvuruga kazana na kufanya yako.
5. Chagua kuangali na kufanyanya yake yakupayo furaha.

Kama unatatizo linalopelekea kukosa furaha na maendeleo ya nafsi yako njoo tuzungumze simu 0755200023


Tuesday, May 4, 2021

MSHAURI AKIKUPA MAJIBU HAYA NI KWAMBA HANA MSAADA UNAOHITAJI

 FOLLOW INSTAGRAM @vivinavisavyake



Wengi wetu tumeshapitia changamoto za kimahusiano ambapo kumueleza mtu tunayemuamini huwa inatupa ahueni au msaada ambao utatuvusha.

Kama huyo unayemuamini na kumwendea kumueleza anakupa majibu haya ina maanisha kwamba aidha jambo lako ni kubwa sana kwake kuweza kulichakata na kukushauri cha kufanya ama hataki kujishuhulisha nalo.

Hivyo anaweza kukupa baadhi au mojawapo ya sentensi hizi. 
1. Kila kitu kinatokea kwasababu.
2. Liombee tu
3. Muda utasema
4. Achana nalo
5. Usiliongelee tena
6. Utakua sawa ukijaribu kulisahau
7. Acha kulifikiria utajisikia vizuri
8. Kuwa imara tu
9. Maisha ndivyo yalivyo
10. Ambacho hakijakuua kinakufanya imara
11. Ingeweza kuwa mbaya zaidi.

Ukishaona majibu hayo hapo juu, aga tu kwa uzuri na usirejee kwake kwani hutapata msaada unaotaka.
Muhimu ni kwakuwa umeshajua basi usikate tamaa bali tafuta msaada kwingine.

Kama una changamoto ya mahusiano njoo tuzungumze simu 0755200023

 


Tuesday, April 27, 2021

FAHYMA ATANGAZA RASMI KUACHANA NA RAYVANNY: Namna ya Kusonga Mbele Pale Penzi Linapoisha

 follow instagram @vivinavisavyake



Kifo cha mahusiano yaliyokuwa ya maana na ya muda mrefu hakina tofauti sana na kifo cha binadamu. 

Tena unaweza kusema huenda kifo cha binadamu kina angalau kwa kuwa baada ya kuomboleza ni kwamba hautawasiliana wala kumuona tena binadamu huyo duniani. 

Kifo cha mahusiano na mtu ambaye mmezaa kinauma kwa wote wawili yani muacha na muachwa au hata iwe ni kuachana yaani wote kukubaliana kwamba hapa mambo hayaendi tena hivyo tusambaratike tu.

Hivyo basi, inawezekana vipi kusonga mbele baada ya kifo cha mapenzi. Fanya yafuatayo

1. Omboleza. 

Yani omboleza hadi umalize ukitoka hapo ni baibai mbele kwa mbele na maisha

2. Jijenge zaidi kiuchumi. 

Hii itakusaidia kuwa busy na shughuli zako hivyo kutokupa muda wa bure wa kumuwaza mpenzi mlieachana.

3. Usimsema vibaya kwa watu na mbele ya jamii. 

Hii inahusika sana hasa kama mmezaa kwani mnahitaji bado kuwa na mawasiliano na mahusiano mazuri kwa ajili ya mlezi wa mtoto wenu.

Mbinu nyingine njoo tuongee ili uweze ku move on mazima. Simu0755200023

Monday, April 26, 2021

Dida Achumbiwa

follow instagram @vivinavisavyake




Mtangazaji wa kipindi cha mashamsham mrembo Dida Shaibu wa radio wasafi amechumbiwa.

Dida amekua ni mrembo mwenye bahati ya ndoa ambapo ameshapitia ndoa kadhaa kama pia ilivyo kwa watu wengine maarufu mfano Shilole na Hadija Kopa. 

Mdau je, ni muda gani ukiwa na mpenzi ukiona hamvalishani pete utabwaga manyanga?

NIMEREJEA WAPENZI

Nifollow instagram @vivinavisavyake

Hatimaye viblog vyetu na vi you tube vya kupost kazi zetu vimerejea tena. Karibuni tena wapendwa wangu tuyadadavue mahusiano na visa vyake vyote.